Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhi Tuzo kwa washindi wa miradi ya ubunifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inayotekelezwa na jamii za asili (wazawa) kutoka sehemu mbalimbali duniani katika shindano linaloratibiwa na Taasisi ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi Duniani (GCA). Tuzo hizo zimekabidhiwa kando ya Mkutano wa 29 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan. Leo tarehe 13 Novemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa washindi wa miradi ya ubunifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inayotekelezwa na jamii za asili (wazawa) kutoka sehemu mbalimbali duniani katika shindano linaloratibiwa na Taasisi ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi Duniani (GCA). Hafla hiyo imefanyika kando ya Mkutano wa 29 wa nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan. Leo tarehe 13 Novemba 2024.