Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya NIC Kitaa iliyofanyika Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa Kampeni ya NIC Kitaa iliyofanyika Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge akipeperusha bendera kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya NIC Kitaa iliyofanyika Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti mara baada ya uzinduzi wa Kampeni ya NIC Kitaa iliyofanyika Makao jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa NIC Insuarance Karimu Meshack akitoa maelezo kuhusiana na kampeni ya NIC Kitaa wakati uzinduzi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge akiwa na timu ya wafanyakazi wa NIC wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya NIC Kitaa iliyofanyika Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
*Yazindua Kampeni ya NIC Kitaa ,wenye madai wafike katika kampeni kulipwa kiganjani mwao
Na Chalila Kibuda,Michuzi Blog
NIC Insurance imesema kuwa ina kazi na wajibu wa kutoa elimu ya uelewa bima nchini ikiwa utekelezaji maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya NIC Kitaa Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge amesema kuwa kampeni hiyo itakwenda nchi nzima katika kutoa elimu ya uelewa wa bima.
Amesema kuwa takwimu ya wananchi wa Tanzania wenye uelewa wa kuhusu bima ni asilimia mbili hivyo kazi lengo ni kufikia asilimia tano.
Amesema NIC Kitaa amesema lengo ni kutoa elimu ya bima kwa watanzania waelewe faida na muhimu katika kulinda uwekezaji wa biashara na mali zao.
Amesema wanaingia msimu wa pili wa kampeni wa NIC Kitaa kusogeza huduma kwa wananchi na kuhakikisha elimu ya bima inawafikia wote na kutambua umuhimu wa bima.
“Uelewa wa bima bado uko chini sisi kama Taasisi kongwe yenye msuli mkubwa katika mtaji tunawajibu wa kusaidia serikali kwa sababu bima ni ukusanyaji wa fedha za wananchi ambao wanahisi wakipata majanga wasaidiwe na faida yake inaweza kusaidia uchumi ambao unawekezwa katika taasisi za fedha zikiwemo benki”amesema Mkeyenge
Amesema katika mikakati ya kutoa uelewa wa bima wanakwenda kuongeza mtaji kwenye soko hususan sekta ya bima.
Mkeyenge amesema kutoa elimu hiyo ni kuendeleza sera ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya bima kwa wote na kuhakikisha watanzania wote wanatumia bima.
Aidha aliongeza kuwa kuwa pamoja na kutoa elimu ya kampeni hiyo wataambatisha na kuandikisha bima kwa wateja wapya na kulipa madeni sio lazima waje ofisini wamewasogezea huduma haduma hapo.
Kampeni hiyo itafanyika nchi nzima kwa sasa wameanza na mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Singida.