Shirika la Bima la Taifa (NIC) limeendelea kutoa elimu Kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutumia bima kupitia kampeni ya NIC KITAA Ili kumlinda mwananchi dhidi ya majanga mbalimbali yanayotokea
Kaimu Mkurugenzi wa masoko na mawasiliano (NIC) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ikiwemo bodaboda,na wajasirimali Ili wafahamu umuhimu na lengo la bima kwenye maisha ya ujumla.
Kafiti amesema Rais wa Jamhuri.ya Muungano wa Tanzania DKT Samia Suluhu Hassan anasisitiza wananchi kujiunga katika bima mbalimbali hii inasaidia kutatua changomoto.mbalimbali wakati wa Majanga.
“tunashauri wananchi wenye biashara , wajasirimali ,wakulima na makundi mengine kujiunga na bima ya NIC ambayo ipo chini ya Serikali kwa asilimia mia Moja”
Kafiti amesema kuwa kuna haja kubwa ya kuhakikisha kila mwananchi anaelewa faida za bima aidha amesisitiza kuwa bima ni msingi wa ulinzi wa kifedha kwa familia na biashara, na kwamba kupitia kampeni hii, wanatarajia kuwafikia watu wa kada zote na kuwasaidia kuelewa umuhimu wa kuwa na bima kama njia ya kujihadhari dhidi ya hasara zinazoweza kutokea.
Kwa upande wake Fredrick Somoni kaimu Meneja wa shirika la bima la taifa mkoa wa Morogoro (NIC) amesema kuwa kampeni hii imelenga kuufikia mkoa mzima wa Morogoro na kwamba itaweza kuwafikia watu wa aina zote, hata wale wa kipato cha chini. Alibainisha kuwa lengo kuu ni kuhakikisha kila mwananchi, bila kujali hali ya kiuchumi, anapata nafasi ya kufahamu kuhusu bima na kufaidika na ulinzi wa kifedha unaotolewa na huduma hizo.
Kampeni hii inalenga kuwapatia wananchi elimu kuhusu faida za kuwa na bima na namna inavyoweza kusaidia kukabiliana na changamoto za kifedha zinazotokana na majanga na uharibifu wa mali
Nao baadhi ya wannachi waliofikiwa na elimu hiyo wamesema Kuna kila haja ya kupewa elimu mara Kwa mara Ili kutambua umuhimu wa bima .
The post NIC watekeleza agizo la Rais Samia watoa elimu ya bima kwa jamii first appeared on Millard Ayo.