Na Oscar Assenga,Handeni.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam ( Dawasa) kuhakikisha wananchi wa eneo la Manga wilayani Handeni mkoani Tanga ambao hawajaunganishwa na huduma ya Maji waunganishiwe kwa mkopo na walipie kidogo kidogo kupitia bili yao.
Agizo la Waziri Aweso alilitoa Leo wakati aliposimama eneo la Manga mpakani mwa Tanga na Pwani lilolopo eneo la Handeni ambapo alisema ni lazima wahakikishe wanapata huduma ya maji na salama wakati wote ili kuondokana na changamoto waliokuwa wanakumbana nayo awali.
Alisema kwamba hilo ndio itakuwa suluhu ya changamoto ambazo walikuwa wakikutana nazo wananchi wa eneo la Manga kwa muda mrefu ya Maji lakini kwa sasa wanachohitaji ni maboresho hivyo dawasa wahakikishe wanabaki eneo hili kutatua changamoto hiyo waone namna gani wanaweza kufanya maboresho ili maji yafika kwa wananchi.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo la mradi wa Tenki eneo la Manga yenye ujazo wa lita lakini tano ambapo alisema maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhi ni kutumia vyanzo toshelevu kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji maeneo mengi maji.
“Ukishafika Manga na Kuna eneo kubwa Mkata maelekezo kwa Dawasa na mtu wa mfuko wa maji awasiliane na Katibu mkuu na mimi nitawasiliana naye wabane fedha Milioni 500 kazi ianze wanamkata watumia maji kutoka mto wami na mkiongeza na maji haya tutakuwa na maji ya uhakika ikiwemo wa bwawa hayo ndio maelezo ya Rais “Alisema Waziri Aweso.
Awali akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian akizungumza baada ya kushuka kwenye Tenki kubwa la maji yanayotokea mto wami kwa ajili ya kusambazwa kwa wananchi kwa ajili ya matumiIzi alisema watu Tanga hawana deni na Rais Dkt Samia Suluhi.
Alisema kutokana na uwepo wa maboresho makubwa katika sekta zote ikiwemo maji ambapo walikuwa na changamoto za maji toka ameingia wameendelea kutatua lakini Waziri Aweso umeemdelea kuwa kinara wa ubunifu katika miradi ya Tanga Uwasa inasifika Duniani kwa ubunifu wako kupita Tanga Wizara yako Tanga Uwasa wamepata fedha ya mtaji wa Bilioni 53 na kuweza katika miradi ya mazingira vyanzo vya maji na miundombinu .
Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando alisema wilaya ya Handeni kwa wilaya hiyo hivi sasa ni kipind kiangazi kikali na kuwepo na upungufu mkubwa wa maji kwenye wilaya hiyo kutokana na vyanzo vingi vya maji kukauka na wanaendelea kulitatua na wamewaambia wananchi wachote maji kwenye vyanzo ramso na wasochote kwenye madimbwi na maji wayachemshe ili kuepukana na madhara ya magonjwa ya tumbo yaliyojitokeza baadhi ya maeneo ikiwemo Kwaleguru.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo mkazi wa Manga Jasmini Shija alisema wanashukuru kwa mradi huo maana walikuwa wanateseka kwa kutembea umbali wa kilomita 300 kufuata maji hivyo uwepo wa mradi huo imekuwa mkombozi mkubwa kwao