Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Ileje, Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza na wananchi wa Jimbo la Ileje mkoani Songwe ailpokuwa akikagua miradi ya maendeleo jimboni kwake Novemba 16, 2024.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Ileje, Mhandisi Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo kwa wazee wa Ileje mkoani Songwe alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo jimboni kwake Novemba 16, 2024.
Baadhi ya Wazee wa Ileje mkoani Songwe wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Ileje (hayupo pichani) alipozungumza nao mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake Novemba 16, 2024.
Muonekano wa kituo cha Afya cha Ndola wilayani Ileje ambapo ujenzi wake umekamilika na kimeanza kutoa huduma kwa wananchi.
Muonekano wa barabara na shamba la Miti la Iyondo Mswima katika mlima wa Katengele linalosimamiwa na Wakala wa Misitu nchini (TFS) ambalo ni chanzo cha ajira na mkakati wa kukuza uchumi na kulinda mazingira jimboni wilayani Ileje Mkoani Songwe.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Ileje, Mhandisi Godfrey Kasekenya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wazee wa Ileje mkoani Songwe mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake Novemba 16, 2024.
…………………
Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Ileje, Mhandisi Godfrey Kasekenya amewahakikishia wazee wa Wilaya ya Ileje kuwa miradi ya miundombinu ya barabara, maji, umeme, shule, zahanati na vituo vya Afya inayoendelea kujengwa jimboni humo itakamilika kwa wakati.
Akizungumza Novemba 16, 2024 wilayani Ileje Mkoani Songwe na wazee hao katika ziara ya kukagua miundombinu inayoendelea kujengwa jimboni humo Naibu Waziri Kasekenya amaesema Serikali imedhamiria kuifungua wilaya ya Ileje katika nyanja zote za miundombinu ili kukuza uchumi katika wilaya hiyo kongwe.
“Wazee wangu Serikali imejipanga kuhakikisha miradi ya miundombinu inajengwa, hivyo wahamasisheni vijana kuchangamkia fursa ajira na uwekezaji katika miradi hii”, amesema Mhandisi Kasekenya.
Aidha, Kasekenya amezungumzia umuhimu wa wazee wilayani humo kutoa elimu kwa vijana kuhusu umuhimu wa kupanda miti na kuitunza ili kulinda uoto wa asili na kunufaika na fursa za kilimo cha miti na uuuzaji wa miti na mbao ambao utakuza uchumi wa Ileje na Taifa kwa ujumla.
Kasekenya amesisitiza kuwa Wilaya ya Ileje itaendelea kufunguliwa kwa miundombinu ya barabara zitakazopitika wakati wote ili kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji wilayani humo.
Kwa upande wake, Mchungaji Msokwa Saston akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake amemshukuru na kumpongeza Mbunge wa Ileje kwa namna anvyothamini wazee na kuwashirikisha katika mipango ya maendeleo na utunzaji wa mazingira na kumuahidi kumpa ushirikiano ili kuhakikisha matarajio ya wanaIleje yanafikiwa.
Ziara ya kutembelea Miundombinu wilayani ileje ni sehemu ya mkakati wa Mbunge huyo kushirikisha makundi mbalimbali ya kijamii kuona kazi zinazofanywa na Serikali wilani humo.