POLISI
Kata ya Ikoma Tarafa ya Grumet Wilayani Serengeti mkoani Mara CPL
Emmanuel Mwikwabe amekabidhi kiti mwendo kwa mtoto Vaileth Enock(16)
mwenye ulemavu wa kuzaliwa ambapo umesababisha kupooza.
Akizungumza
wakati akikabidhi kiti mwendo hicho ,CPL Mwikwabe amesema alimbaini
Mtoto huyo kupitia kampeni ya utoaji wa elimu ya Polisi Jamii Elimu
Nyumba kwa Nyumba katika Kijiji cha Parknyigoti katika kitongoji cha
Park B kupitia baba yake mzazi Mzee Enonck Komanya.
“Nilifanikiwa
kufika nyumbani kwa Mzee Enonck Komanya nakuwakuta watoto wake na
miongoni mwa watoto niliowakuta kwenye mji huo ni pamoja na binti huyu
Vaileth , hivyo nikaamua nimshirikishe Mkuu wa Wilaya Bi.kemirembe na
kukubali kunishika mkono kwa kunipa kiti mwendo,amesema CPL Emanuel
Mwikwabe.
Pia
amesema amekabidhi kiti hicho kwa lengo la kupeleka faraja kwa mtoto
huyo ambaye toka azaliwe amekuwa akiishi kwa kulala kutokana na kukosa
kiti mwendo.
Ametumia
nafasi hiyo kuwa kuwataka Wazazi pamoja na wakazi katika kata hiyo
kuacha kuwabagua watoto wenye ulemavu waliopo kwenye maeneo yao kwani
kufanya hivyo nikuwafanyia ukatili