Kufuatia juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuanzisha huduma za Madaktari Bingwa wanaozunguka mikoa mbalimbali nchini, wakazi wa Mkoa wa Mara wameomba mpango huo uwe endelevu, wakibainisha kuwa umekuwa msaada mkubwa kwao.
RC Mara Awapokea Madaktari 42 Bingwa
Kufuatia juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuanzisha huduma za Madaktari Bingwa wanaozunguka mikoa mbalimbali nchini, wakazi wa Mkoa wa Mara wameomba mpango huo uwe endelevu, wakibainisha kuwa umekuwa msaada mkubwa kwao.
Kauli hiyo ilitolewa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, wakati akiwapokea Madaktari Bingwa 42 katika Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, maarufu kama Kwangwa.
Wakazi wa Manispaa ya Musoma wamesema ujio wa madaktari hao umewaondolea gharama kubwa za matibabu, ambazo awali walilazimika kuzifuata katika hospitali za Bugando, KCMC, na Muhimbili.
Kanali Mtambi amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Mara kutumia siku sita za uwepo wa madaktari hao kupata huduma za kibingwa ili kuboresha afya zao.
“Awali, hali ilikuwa ngumu; mtu alilazimika kusafiri kilomita nyingi kwa gharama kubwa. Leo huduma hizi zimeletwa mlangoni. Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa ubunifu huu,” alisema Kanali Mtambi.