Wazairi wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza jambo leo Disemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024), lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu akizungumza jambo leo Disemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024), lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Husna Sekiboko akizungumza jambo leo Disemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024), lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Baadhi ya Wabunifu wa Sayansi na Teknolojia pamoja na wadhamini wa Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024) wakipewa vyeti na Wazairi wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda kama sehemu ya kutambua mchango wao katika sekta ya sayansi.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024) wakifatilia jambo katika kongamano hilo.
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Wazairi wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ili kuwawezesha vijana wa kitanzania kuona sekta hiyo kama fursa ya maendeleo.
Akizungumza leo Disemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024), lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Profesa Mkenda, amesema kuwa mfuko wa samia ambao umezinduliwa katika kongamano hilo umelenga kusaidia wabunifu kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza bunifu zao ziweze kusaidia kuboresha maisha ya jamii na kukuza uchumi wa Nchi.
Profesa Mkenda amesisitiza umuhimu wa wabunifu kutumia maarifa waliyopata katika kongamano hilo ili kuhakikisha sayansi na ubunifu havibaki kwenye maabara bali vinsaidia kubadilisha maisha ya watazania.
Amesema kuwa serikali itaendelea kutoa msukumo ili kuhakikisha sayansi inakuwa mhimili wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.