Naibu Waziri wa fedha Othman Chande ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha Dkt.Mwingulu Nchemba akizungumza katika mahafali ya 84 ya wachungaji katika chuo cha International Evangelism Church kilichopo Sakila mkoani Arusha.

Askofu wa makanisa ya International Evangelism Church Tanzania,Dkt Eliud Issagya akizungumza katika mahafali hayo mkoani Arusha .

…………
Happy Lazaro, Arusha .
Wahitimu wa Chuo cha biblia Sakila wametakiwa kutumia nafasi zao vizuri katika kukemea swala la maadili na malezi katika maeneo yao sambamba na kuacha tamaa kwani huo ndio msingi ulio bora.
Hayo yamesemwa na leo na Naibu Waziri wa fedha Othman Chande ambaye amemwakilisha Waziri wa fedha Dkt.Mwingulu Nchemba katika mahafali ya 84 ya wachungaji katika chuo cha International Evangelism Church kilichopo Sakila mkoani Arusha ambapo jumla ya wahitimu 73 wamehitimu kozi ya biblia chuoni hapo.
Chande amesema kuwa, endapo wachungaji watatumia nafasi zao ipasavyo itasaidia sana kupunguza maovu mbalimbali.katika.jamii ikiwa ni pamoja na kuhubiri amani katika jamii.
“Nawaombeni sana muepukane na rushwa katika kazi zenu kwani ndio inapelekea kuwa na tamaa na kusababisha watu kutoka kwenye msingi ya maadili badala yake nyie mkawe mstari wa mbele na mabalozi katika kukataa na kukemea rushwa “amesema .
“Baba Askofu nakupongeza sana kwa kitendo ulichofanya cha kuanzisha chuo hiki kwani ni jambo kubwa sana na kwa kufanya hivyo umelitendea haki neno la Mungu .’amesema
Aidha Chande amewataka wachungaji kuhubiri haki katika maeneo yao na wawe na mapenzi ya dhati na wasiwe na tofauti na wenzao badala yake waendelee kupendana na kutenda haki kwa kila mmoja .
Chande amewataka kutumia nafasi zao vizuri katika kuepuka wivu,choyo na husda kwani.hizo ndizo zina madhara makubwa katika.maisha ya mwanadamu .
“Serikali inatambua kwa kiwango kikubwa sana mchango wa taasisi za dini kwani zinafanya kazi nzuri sana ya kusaidia serikali na sisi tupo pamoja katika kuhakikisha malengo yao yote yanafikiwa.,
“amesema Chande .
Naye Askofu wa makanisa ya International Evangelism Church Tanzania,Dkt Eliud Issagya amesema kuwa, chuo hicho kina miaka 41 sasa tangu kuanzishwa kwake ambapo kimekuwa kikitoa kozi ya uchungaji.
Amesema kuwa,wao kama viongozi wa dini wamekuwa wakishirikiana na serikali katika kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kwani zimekuwa zikiharibu vijana wengi ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Askofu Dkt.Issagya amewataka wahitimu hao kuendeleza vipaji vyao walivyopata katika kuisaidia jamii katika maswala mbalimbali ikiwemo kuhubiri amani na upendo katika jamii inayowazunguka.
Naye Mmoja wa wahitimu akisoma risala, Richard Meru amesema kuwa mbali.na masomo.ya biblia chuo hicho kimeweza kutoa elimu kuhusu kazi za mikono na kuweza kuwaandaa kuwa wachungaji wazuri ambao watahudumia jamii katika nyanja mbalimbali .