Na Farida Ramadhani,WF, Dar es Salaam
Serikali
ya Tanzania na Shirika la Maendeleo La Ufaransa (AFD) wamesaini
mikataba minne (4) yenye jumla ya euro milioni 118.8 sawa na takriben
shilingi bilioni 323.4 kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali nchini
ikiwemo Awamu ya Pili ya mradi wa nishati jua wa Kishapu Mkoani
Shinyanga, pamoja na uendelezaji wa misitu na utunzaji wa hifadhi ya
misitu ya mikoko.

Hafla
ya utiaji saini wa Mikataba hiyo imefanyika jijini Dar es Salam kati ya
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kwa upande wa
Serikali na Naibu Balozi wa Ufaransa nhini Tanzania, Mhe. Axel-David
Guuillon pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD),
Bi. Celine Robert.

Akizungumza
baada ya kusaini Mikataba hiyo, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameck Nchemba alisema katika Mikataba hiyo iliyosainiwa euro milioni
75.9 ni kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Nishati ya
jua unaotekelezwa Kishapu Mkoani Shinyanga.

Alisema
kuwa mradi huo utazalisha Megawati 150 ambapo Awamu ya Kwanza upo
katika hatua za utekelezaji na unatarajiwa kuzalisha Megawati 50 na
Awamu ya Pili ambayo mkataba wake umesainiwa inatarajiwa kuzalisha
Megawati 100 na kufanya jumla ya Megawati zitakazozalishwa kuwa 150.

‘’
Kuingiza Megawati 150 kwenye gridi ya Taifa, kutapunguza utegemezi wa
nishati ya nguvu za maji ambayo inaathirika kwa kiasi kikubwa kutokana
na mabadiliko ya tabianchi. Mradi huu utaongeza upatikanaji wa nishati
ya uhakika katika Mkoa wa Shinyanga ambao una umuhimu wa kimkakati wa
kiuchumi na kijamii kutokana na kuwepo kwa shuhguli kubwa na ndogondogo
za uchimbaji madini” alibainisha Mhe. Dkt. Nchemba.

Mkataba wa pili wa Euro milioni 39.9 ni kwa ajili ya uendelezaji wa
mashamba ya misitu na utunzaji wa hifadhi ya mikoko ili kuongeza wigo wa
upandaji miti, kuboresha ubora na wingi wa mbegu za miti na kuboresha
usimamizi wa mbegu hizo.

mradi huo utaimarisha vituo vya kukusanya mbegu za miti na kuanzisha
vitalu vya kisasa vya miti ikiwa ni pamoja na kutaboresha utunzaji wa
hifadhi ya misitu ya mikoko, kuboresha uhifadhi wa uhasilia wa mazingira
na kuchangia kuinua utalii na kuboresha Maisha ya jamii.

Dkt.
Nchemba alisema mikataba ya euro milioni 2 ni kwa ajili ya utunzaji wa
hifadhi ya mikoko na euro milioni 1 ni kwa ajili ya kufadhili Mpangokazi
wa Jinsia unaotekelezwa na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO),
chini ya mradi wa uendelezaji wa nishati ya Jua.

“Huu
ni mwendelezo wa ushirikiano wetu mzuri ambao umeshuhudiwa kwa kuwepo
kwa miradi mbalimbali ambayo inafadhiliwa kwa mikopo nafuu kutoka
Serikali ya Ufaransa kupitia AFD”, alisema Mhe. Dkt. Nchemba.

kuwa Serikali ya Ufaransa kupitia AFD imefadhili miradi mbalimbali
kupitia mikopo nafuu katika sekta za Nishati, Maji, Usafirishaji na
Kilimo ambayo mingine inaendelea na mingine imekamilika.

Naye
Kaimu Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Axel-David Guuillon alisema
miradi itakayotekelezwa kupitia mikataba hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya
nchi kwa kuwa itasaidia kupunguza gharama za kuagiza mafuta pamoja na
kuhifadhi mazingira.

Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD),
Bi. Celine Robert, alisema kuwa mikataba hiyo ni mwendelezo wa uhusiano
uliopo kati ya Tanzania na Shirika hilo.

mkataba wa kuendeleza misitu nchini utaiwezesha Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS), kujumuisha ukuaji wa uchumi, ushirikishwaji wa
jamii na utunzaji endelevu wa mazingira.

Bi.
Robert alisema mkataba wa Awamu ya Pili ya mradi wa nishati ya jua
Kishapu Mkoani Shinyanga, utaiwezesha nchi kukabiliana na changamoto za
umeme kwa kuwa Tanzania itakuwa na vyanzo tofauti tofauti vya umeme.

“Mabadiliko
ya hali ya hewa yapo na yanaathari nyingi siku za usoni, mradi huu wa
umeme utaiwezesha Tanzania kukabiliana na tatizo la umeme hususani
yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na kutunza mazingira”
alisema. Bi. Robert.

upande wa Manaibu Mawaziri wa Sekta ambazo zitatekeleza miradi hiyo
walisema watasimamia kikamilifu miradi hiyo ili kuhakikisha inafikia
malengo kusudiwa ambapo Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga
alisema mkataba wa Awamu ya Pili ya mradi wa nishati ya jua Kishapu
Mkoani Shinyanga ni mradi muhimu ambao unaenda kuchagiza miradi mingine
ambayo inazalisha nishati jadidifu ambazo zinapunguza athari za
mazingira.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula, alisema
fedha hizo zilizosainiwa katika mikataba hiyo zitatumika kupanda miti na
kusimamia misitu ya mikoko.

mikataba hiyo itaiwezesha nchi kukabiliana na athari za mabadiliko ya
tabianchi pamoja na kuongeza uwezo wa kuvuna mazao yanayotokana na
misitu

Waziri
wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), (Katikati),
akisaini mikataba minne (4) yenye jumla ya euro milioni 118.8 sawa na
takriban shilingi bilioni 323.4 kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali
nchini ikiwemo Awamu ya Pili ya Mradi wa Nishati-jua wa Kishapu Mkoani
Shinyanga pamoja na uendelezaji wa misitu na utunzaji wa Hifadhi ya
Misitu ya Mikoko, zilizotolewa na Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika
lake la Maendeleo (AFD), Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Balozi wa
Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Axel-David Guuillon na kushoto ni
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Celine Robert.

akibadilishana na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD),
Bi. Celine Robert, moja kati ya Hati Nne za Mikataba yenye jumla ya euro
milioni 118.8 sawa na takriban shilingi bilioni 323.4 zilizotolewa na
AFD, kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo Awamu ya Pili
ya Mradi wa Nishati-jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga pamoja na
uendelezaji wa misitu na utunzaji wa Hifadhi ya Misitu ya Mikoko,
Anayeshuhudi kulia ni Naibu Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe.
Axel-David Guuillon, Jijini Dar es Salaam.

wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), Katikati),
Naibu Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Axel-David Guuillon
(kulia) na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi.
Celine Robert, wakionesha Hati za Mikataba yenye jumla ya euro milioni
118.8 sawa na takriban shilingi bilioni 323.4 zilizotolewa na AFD, kwa
ajili kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo Awamu ya Pili ya Mradi
wa Nishati-jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga pamoja na uendelezaji wa
misitu na utunzaji wa Hifadhi ya Misitu ya Mikoko, Jijini Dar es Salaam.

akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania na
Ufaransa baada ya kuia Saini Hati za Mikataba Minne (4) yenye jumla ya
euro milioni 118.8, sawa na takriban shilingi bilioni 323.4 zilizotolewa
na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), kwa ajili kutekeleza miradi
mbalimbali nchini ikiwemo Awamu ya Pili ya Mradi wa Nishati-jua wa
Kishapu Mkoani Shinyanga pamoja na uendelezaji wa misitu na utunzaji wa
Hifadhi ya Misitu ya Mikoko. kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Danstun Kitandula, kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.
Judith Kapinga, wa pili kulia ni Naibu Balozi wa Ufaransa nchini
Tanzania, Mhe. Axel-David Guuillon na wa pili kushoto ni Mkurugenzi
Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Celine Robert na
Maafisa wengine wa Serikali kutoka Tanzania na Ufaransa. Tukio hilo
limefanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF, Dar es Salaam)