-Akabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya mamilioni ya fedha katika Jimbo la Chwaka
MWAKILISHI
wa Jimbo la Chwaka visiwani Zanzibar ambaye pia ni Katibu wa
Halmashauri Kuu((NEC) Oganaizesheni Issa Gavu amesema Serikali ya Awamu
ya Nane chini ya Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi imefanya maendeleo makubwa
kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu.
Sambamba na hayo
amesema wananchi wa Jimbo la Chwaka wameendelea kushuhudia changamoto
mbalimbali zikipatiwa ufumbuzi pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya
barabara,elimu,afya na maji huku akielezea wazi Chama Cha Mapinduzi
(CCM) ndicho kilichokuwa na uthubutu na utayari wa kuwatumikia wananchi.
Gavu
ameyasema hayo leo Desemba 14,2024 alipokuwa akielezea utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo la Chwaka ambapo pia amekabidhi
pikipiki 20 zenye thamani ya Sh.milioni 72 , Vifaa vya michezo vyenye
thamani ya Sh.milioni 17.
Pia amekabidhi vitenge ,fulana na
kofia vyenye thamani ya Sh.milioni 14 , michango kwa jamii milioni
22,vyarahani 100 thamani ya Sh.milioni 30,bati,saruji na vifaa vya
ujenzi vyenye thamani ya Sh.milioni Saba pamoja na mashine 15 za
kuprintia ambapo kila Moja thamani ni zaidi ya Sh.milioni 2.1.
Akieleza
zaidi amesema hana shaka katika uchaguzi ujao viongozi kuanzia diwani,
Mbunge na Mwakilishi pamoja na Rais watatoka Chama Cha Mapinduzi huku
akifafanua kuna vyama 19 lakini hakuna chama, jumuiya wala taasisi yenye
utayari na uthubutu wa kuweza kuliongoza Taifa letu kwa mfanisi na
mafanikio makubwa kama wanayoyaona kwa Chama Cha Mapinduzi.
“Sisi
watu wa Chwaka ni mashahidi na ni mashuhuda kwenye serikali hii ya
Awamu ya nane yako mambo yalikuwa yanatukwaza , Serikali hii ya CCM
chini ya uongozi wa Dk.Hussein Ali Mwinyi tumepiga hatua kubwa sana
katika maendeleo ndani ya watu wa Jimbo la Chwaka
“Yapo maeneo
tulikuwa na changamoto za maji , elimu ,afya sambamba na miundombinu
lakini leo hii jitihada na mipango ya Serikali kila mmoja wetu anaiona
kama haijakamilika basi iko kwenye mchakato,kama haiko katika mchakato
iko katika mfumo wa kutafuta utaratibu mzuri wa kufanikisha kuondoa
changamoto hizo.
“Tunayo miradi ya kitega uchumi kwa ajili ya
kuwezesha wajasiriamali, tunavyo vyuo vya ufundi pamoja na vituo vya
elimu,hayo yote ni matunda ya kukichagua Chama Cha
Mapinduzi.Ninachokuombeni watakapokuja wenzetu kuja kuzungumza nanyi
msiwakasirikie wala msigombane nao.
“Sisi hoja yetu tutakwenda
kuijibu kwa vitendo lakini tunawajibu wa kujiandaa vizuri na
utakapofika wakati wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura Jimbo
letu liwe na malengo ya kufikia ufanisi kwa asilimia 100 katika
uboreshaji wa daftari la kupiga kura,”ameelezea Gavu.
MWAKILISHI wa Jimbo la Chwaka visiwani Zanzibar ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu((NEC) Oganaizesheni Issa Gavu,akikabidhi pikipiki 15 zenye thamani ya Sh.milioni 72 , Vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh.milioni 17. leo Desemba 14,2024 alipokuwa akielezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo la Chwaka.
MWAKILISHI wa Jimbo la Chwaka visiwani
Zanzibar ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu((NEC) Oganaizesheni
Issa Gavu, Akizungumza leo Desemba
14,2024 alipokuwa akielezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu katika
Jimbo la Chwaka ambapo pia amekabidhi pikipiki 15 zenye thamani ya
Sh.milioni 72 , Vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh.milioni 17.