wamejengewa uwezo wa masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) na Kampuni ya simu ya Mikononi ya Vodacom Tanzania tangu 2018
mpaka mwaka huu kupitia program ya Code Like a Girl
Mkuu wa
Kanda ya kati wa Vodacom Tanzani, Joseph Sayi alisema hayo leo desemba
13 wakati alipokuwa akifunga mafunzo hayo ya TEHAMA yaliyofanyika Chuo
kikuu cha Dodoma (Udom).
Alibainisha kuwa mafunzo hayo yamekuwa
yakitolewa kwa awamu kwa baadhi ya Mikoa hapa nchini yakiwa na lengo la
kuwajengea uwezo wa masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati
(STEM) wanafunzi hao wa kike kwa ufadhili wa Vodacom Tanzania PLC.
Meneja
wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati Joseph Sayi (kushoto)
akimkabdhi cheti mwanafunzi Winnie Futa wakati wa kufunga mafunzo ya
kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike katika masomo ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofadhiliwa na Vodacom.
wa Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati ,Joseph Sayi
(kulia) akizungumza na wanafunzi wasichana kutoka Kanda hiyo wakati wa
kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masomo ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Udom Jijini
Dodoma jana kwa ufadhili wa Vodacom.
Meneja
wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati Joseph Sayi (kushoto)
akimkabidhi begi mwanafunzi Emmeline Kitali wakati wa kufunga mafunzo
ya kuwajengea wanafunzi wa kike uwezo wanafunzi wa kike katika masomo
ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofanyika Chuo
kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhiliwa na Vodacom.
Baadhi
ya wanafunzi wa kike kutoka shule za sekondari Kanda ya kati
wakijifunza jinsi ya kutumia kopyuta kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo
katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA )
yaliyofanyika Chuo kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhili wa
kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania.