Na MWANDISHI WETU,
elimu ya hifadhi ya jamii kwa makundi mbalimbali ya wananchi
linaendelea kwa kasi baada ya wajasiriamali katika soko ya Tegeta Nyuki,
jijini Dar es Salaam, kuhamasika kujiwekea akiba baada ya kupata elimu
kutoka NSSF ili waweze kunufaika na mafao.
NSSF kupitia kwa
Meneja wa Sekta isiyo rasmi, Bi. Rehema Chuma imeweka kambi ya siku nne
katika soko la Tegeta Nyuki na Kawe, lengo likiwa ni kutoa elimu ya
hifadhi ya jamii, kuandikisha wanachama wapya na kuhamasisha uchangiaji
ambapo hamasa ya wajasiriamali kupata elimu na kujiunga imekuwa kubwa.
Akizungumza
tarehe 8 Januari 2025, Bi. Rehema amesema katika muendelezo wa utoaji
elimu kwa wajasiriamali NSSF imefika katika soko la Tegeta Nyuki kwa
ajili ya kufikisha elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na
kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.
Amesema
kuna namna mbili za mwanachama kujiunga moja wapo ni kujaza fomu na
mwenye namba ya NIDA anaelimishwa kujisajili kwa kutumia mifumo, na kuwa
mwanachama anaweza kuwasilisha michango kupitia simu ya kiganjani huko
huko aliko ambapo kima cha chini cha kuchangia ni shilingi 30,000 ambapo
atanufaika na fao la matibabu.
Baadhi ya wajasiriamali akiwemo
Pastory Anthony ambaye ni mwanachama wa NSSF ananufaika na mafao
yanayotolewa na Mfuko ikiwemo ya matibabu pamoja na familia yake.
Amesema
kuna faida nyingi ambazo anazipata kwa kuwa mwanachama wa NSSF hivyo
amewaomba wajasiriamali wengine kujiwekea akiba NSSF kwani ni mkombozi
kwa kila mwanachama.
Naye, Bw. Marc Donald Maganga, Afisa Mkuu wa
Sekta isiyo rasmi, amesema NSSF imeweka utaratibu nzuri wa
wajasiriamali kujiunga na kuchangia ambapo mwanachama baada ya
kujiandikisha anapewa namba ya kumbukumbu ya malipo na anapaswa
kuchangia kuanzia shilingi 30,000 au 52,200 au zaidi kwa mwezi na
anaweza kuchangia kidogo kidogo kwa siku, wiki, mwezi, muhula au msimu
ili aweze kunufaika na mafao yote yanayotolewa ikiwemo ya uzee, urithi,
uzazi, matibabu na msaada wa mazishi.