Na. Saidina Msangi na Asia Singano, WF, Dodoma
Serikali
imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Shirika la Fedha la Kimataifa
(IMF), na kuhakikisha Fedha zote za maendeleo zinazotolewa na Shirika
hilo zinatumika kukamilisha azma ya kukuza uchumi wa nchi.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb),
jijini Dodoma wakati akimuaga Kiongozi wa Timu ya Wataalam ya Shirika la
Fedha la Kimataifa (IMF) kwa Tanzania, Bw. Charalambos Tsangarides,
aliyemaliza muda wake baada ya kuhudumu kwa zaidi ya miaka mitatu na
nusu.
Alisema Serikali itaendelea kutekeleza dhamira yake ya
kuwaletea wananchi maendeleo na kukuza uchumi kwa ujumla kupitia juhudi
mbalimbali inazofanya ikiwemo kutafuta fedha za kutekeleza miradi
mbalimbali ya kimkakati.
‘Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania,
napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kujitolea kwako katika kusaidia
safari ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu, ninawahakikishia kwamba
Timu yangu itawapa ushirikiano wote unaohitajika, kwa upande mwingine,
nina furaha kuwajulisha kwamba tunaendelea vyema na hatua zetu za
mageuzi chini ya program mpya ya Serikali ya kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabianchi kupitia dirisha la Resilient and Sustainable
Fund (RSF),’’ alisema Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba, mbali na
kumuaga Kiongozi huyo wa IMF nchini, alitumia fursa hiyo kumkaribisha
Kiongozi mpya anayechukua nafasi hiyo Bw. Nicolas Blancher, huku
akimuahidi ushirikiano kutoka Serikali ya Tanzania.
‘’Napenda
kuchukua fursa hii kumkaribisha rasmi Bw. Nicolas Blancher, kama
Kiongozi wetu mpya wa “Mission” kwa Tanzania na tunafurahi kupata nafasi
ya kushuhudia mwongozo kutoka kwa mtaalamu mwingine kama tulivyofanya
na Kiongozi wa “Mission”anayemaliza muda wake katika kufanikisha
maendeleo yetu endelevu ya kiuchumi’’ alisema Dkt. Nchemba.
Kwa
upande wake Kiongozi wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la
Kimataifa (IMF) kwa Tanzania, anayemaliza muda wake, Bw. Charalambos
Tsangarides, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa
alioupata wakati akitekeleza majukumu yake nchini.
Aidha,
ameipongeza Serikali kwa juhudi za kusimamia maendeleo ya kiuchumi na
kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha ustawi wa
wananchi wake hata baada ya kumaliza muda wake wa kuhudumu.
Naye
Kiongozi Mpya wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la Kimataifa
(IMF) Bw. Nicolas Blancher, ameahidi kushirikiana kikamilifu na Serikali
ya Tanzania na kumhakikishia Dkt. Nchemba kuwa ataendeleza ushirikiano
na kazi zilizofanywa na mtangulizi wake huku akisisitiza dhamira ya
kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanatimia.Waziri
wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimkabidhi zawadi
Kiongozi wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw.
Charalambos Tsangarides, anayemaliza muda wake wa kuisimamia Tanzania
baada ya kuhudumu kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu, katika kikao
kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mhe. Waziri wa Fedha, jijini
Dodoma.Waziri
wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiagana na Kiongozi wa
Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Charalambos
Tsangarides, anayemaliza muda wake wa kuisimamia Tanzania, wakati
alipofika kuagana na Waziri Mhe. Dkt. Nchemba pamoja na kumtambulisha
Kiongozi mpya wa Shirika hilo anayechukua nafasi yake, Bw. Nicolas
Blancher, katika ukumbi wa Mikutano wa Mhe. Waziri wa Fedha, jijini
Dodoma.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akisalimiana na
Kiongozi Mpya wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
Bw. Nicolas Blancher, anayeshuhudia ni Kiongozi wa Timu ya Wataalam ya
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Charalambos Tsangarides,
aliyemaliza muda wake na Mwakilishi Mkazi wa IMF, Bw. Sebastian Acevedo,
katika ukumbi wa Mikutano wa Mhe. Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.Waziri
wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa
kikao kifupi akiagana na Kiongozi wa Timu ya Wataalam ya Shirika la
Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Charalambos Tsangarides, anayemaliza muda
wake nchini Tanzania na kumkaribisha Kiongozi Mpya wa Timu ya Wataalam
ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Nicolas Blancher, katika
ukumbi wa Mikutano wa Mhe. Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban, katika kikao
chake na ujumbe wa IMF, katika ukumbi wa Mikutano wa Mhe. Waziri wa
Fedha, jijini Dodoma.
Kiongozi
wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw.
Charalambos Tsangarides, anayemaliza muda wake nchini Tanzania
akizungumza wakati wa kikao kifupi na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameck Nchemba (Mb), wakati alipofika kwa ajili ya kumuaga pamoja na
kumtambulisha Kiongozi Mpya wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la
Kimataifa (IMF) Bw. Nicolas Blancher, katika ukumbi wa Mikutano wa Mhe.
Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
Kiongozi
Mpya wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw.
Nicolas Blancher, akizungumza wakati wa kikao kifupi na Waziri wa Fedha,
Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati alipofika kwa ajili ya
utambulisho, katika ukumbi wa Mikutano wa Mhe. Waziri wa Fedha, jijini
Dodoma.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiwa katika picha ya
pamoja na Kiongozi wa Timu ya Wataalam ya Shirika la Fedha la Kimataifa
(IMF), Bw. Charalambos Tsangarides, anayemaliza muda wake, akifuatiwa na
Kiongozi mpya wa IMF Bw. Nicolas Blancher, na Mwakilishi Mkazi wa IMF,
Bw. Sebastian Acevedo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi.
Amina Khamis Shaaban, Kamishna wa Idara ya Sera Bw. Johnson Nyella, na
Kamishna Msaidizi idara ya Fedha za Nje Bw. James Msina. Kikao hicho
kilifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mhe. Waziri wa Fedha, jijini
Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)