Na Saidina Msangi, WF, Karatu, Arusha.
Serikali
kupitia Wizara ya Fedha, imebainisha kuwa itaendelea na utoaji wa elimu
ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini ili
kuwawezesha wananchi katika maeneo ya vijijini kuwa na uelewa wa elimu
ya fedha pamoja na kuwa na matumizi sahihi ya fedha na kuweka akiba.
Hayo
yamebainishwa na Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji
Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, wakati Timu ya
Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, iliyoambatana na Maafisa kutoka
taasisi na wadau mbalimbali ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya
fedha kwa wakulima, waendesha bodaboda na wafugaji, katika ukumbi wa
mikutano wa Tarafa ya Endabash, wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.
Bw.
Kibakaya alieleza kuwa mfumo wa filamu unaotumiwa kutoa elimu ya fedha
umewavutia wananchi kwa kuwa umekuwa mfumo rahisi utakaowawezesha
kukumbuka kwa urahisi mafunzo waliyopata ya elimu ya fedha.
‘‘Kumekuwa
na mwitikio mkubwa wa wananchi kuhudhuria mafunzo ya elimu ya fedha
inayotolewa kwa njia ya filamu yenye mada mbalimbali ikiwemo uwekaji
akiba, bima, utunzaji wa fedha na mada ya masuala ya uwekezaji wa
masuala ya kifedha,’’ alieleza Bw. Kibaya.
Alisema kuwa Serikali
iliona kuwa ni muhimu kuwapatia wananchi elimu ya fedha ili kuwawezesha
kuwa na uelewa wa elimu ya fedha ikiwa ni pamoja na kuzingatia matumizi
sahihi ikiwemo kutumia vema mikopo inayotolewa na Serikali kuwawezesha
wananchi kiuchumi.
Bw. Kibakaya alifafanua kuwa elimu hiyo ya
fedha italeta mabadiliko kwa wananchi hasa ikizingatiwa kuwa njia ya
uwasilishaji kwa filamu itabaki kuwa kumbukumbu ya muda mrefu hivyo
kuendelea kujenga mabadiliko ya usimamizi wa fedha binafsi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Endabash, Bw. Boisa Mandoo,
aliishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupata elimu ya fedha katika maeneo
yao ambayo itawasaidia katika kusimamia matumizi ya fedha pamoja na
kutumia huduma za fedha zinazotolewa na watoa huduma waliosajiliwa kwa
mujibu wa sheria.
‘’Naipongeza Serikali ya Rais Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kutuletea wataalamu kuja kutoa elimu ya fedha kwa
wananchi na sisi kama Serikali tutaendelea kuzihamasisha taasisi za
fedha ambazo hazijasajiliwa ziweze kusajiliwa ili wananchi waweze kupata
huduma katika taasisi rasmi’’, alisema Bw. Mandoo.
Program ya
kutoa elimu kwa Umma ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo Sekta ya
Fedha 2020/21 – 2029/30 ambapo unalenga kufikia wananchi asimia 80 hadi
kufikia mwaka 2025/26 pamoja na utekelezaji wa Programu ya Elimu ya
Fedha kwa Umma ya mwaka 2020/21 – 2025/26.
Afisa
Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara
ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akitoa ufafanuzi kuhusu namna ya
kusimamia mapato na matumizi, wakati timu ya Maafisa kutoka Wizara ya
Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali,
ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa
huduma za fedha vijijini, katika ukumbi wa mikutano wa Tarafa ya
Endabash, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Endabash, Bw. Boisa Mandoo, akizungumza na wananchi wa
Kijiji hicho, wakati wa kuikaribisha Timu ya Wataalamu wa kutoa elimu ya
fedha kutoka Wizara ya Fedha, iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi
na wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha kwa wakulima,
waendesha bodaboda na wafugaji, katika ukumbi wa mikutano wa Tarafa ya
Endabash, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.
Baadhi
ya wakulima, waendesha bodaboda na wafugaji wa Tarafa ya Endabash,
wakipata elimu ya fedha kwa njia ya filamu, wakati Timu ya Maafisa
kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau
mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha
utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika ukumbi wa mikutano wa
Tarafa ya Endabash, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.
Afisa
Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za
Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, akitoa elimu
ya fedha kuhusu umuhimu wa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa kwa
wakulima, waendesha bodaboda na wafugaji wa Tarafa ya Endabash, wakati
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka
taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya
fedha
Meneja
wa Benki ya NMB Tawi la Karatu, Bw. Edgar Ninga, akitoa ufafanuzi
kuhusu mikopo inayotolewa na Benki hiyo, wakati Timu ya wataalamu kutoka
Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau
mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha
utumiaji wa huduma za fedha vijijini kwa wakulima, waendesha bodaboda
na wafugaji wa Tarafa ya Endabash, katika ukumbi wa mikutano wa Tarafa
ya Endabash, wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.
Afisa
Uandikishaji Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Wilaya ya
Karatu, Bi. Prisca Damiano, akitoa ufafanuzi kuhusu namna ya kujiunga na
Mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa, wakati Timu ya Maafisa kutoka
Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau
mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha
utumiaji wa huduma za fedha vijijini kwa wakulima, waendesha
bodase3dsdboda na wafugaji wa Tarafa ya Endabash, katika ukumbi wa
mikutano wa Tarafa ya Endabash, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF- Karatu, Arusha)