Na Mwandishi Wetu
OFISI ya
Diwani Kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam imetoa taarifa ya
utekelezaji wa Ilani sambamba na kukata keki kwa ajili ya kusherehekea
Happy Birthday ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Usomwaji wa
taarifa hiyo ya utekelezaji wa Ilani pamoja na kukata keki ya Rais
umefanyika leo Januari 26,2025 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa mkoa huo akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa Abbas
Mtemvu.
Wengine waliohudhuria ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Ilala Alhaji Said Sidde pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa na
Naibu Spika Wa Bunge Mhe Mussa Azzan Zungu pamoja na Wajumbe wa NEC Mkoa
akiwemo Juma
Gafafi.
Katika usomaji wa utekelezaji wa
Ilani ofisi ya Diwani Kata ya Kivukoni ambayo Diwani wake ni Sharik
Choughule imejivunia utekelezaji wa Ilani kwani kuna miradi mingi ya
maendeleo imefanya na kutumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Dk.Samia kwa
kuhakikisha anasimama imara oufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
Mkuu 2020-2025.