Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt. Jones Killimbe akitoa hotuba ya ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni, yaliyofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa PSSSF House , tarehe 11 Februari, 2025.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Imeelezwa kuwa Usalama wa mtandaoni ukiimarishwa utasaidia kujenga imani kwa watumiaji wengi na kupanua wigo wa utumiaji wa mtandao hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo Februari 11,2025 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Dkt Jones Killimbe katika maadhimisho ya siku ya usalama mtandaoni 2025 yalioyafanyika jijini Dodoma.
“Sisi sote tulioko hapa ni wadau wa usalama wa mtandao wa internent usalama ukiwepo na kuimarishwa na utajenga imani ya watumiaji wengi zaidi na hivyo kupanua matumizi ya internent,”amesema.
Amesema kuwa watu wakianza kuogopa internent kama shetani taifa litashindwa kujipambanua katika uchumi wa kidijiti kwasababu hawawezi kuepuka huko na kuongeza kuwa taifa likianza kutumia pia akili mnemba kwenye matibabu itwaweza nayo kuwasaidia.
Awali Mwakilishi wa Mkurugnezi mkuu wa TCRA ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Leseni na ufuatiliaji Bw. John Daffa ametaja sababu zinazopelekea watumiaji wa mtandao kuchangia matukio yanayohatarisha usalama mtandaoni.
“Kama tunavyofahamu mtandao hauna mipaka wa kuwazuia watu kutumia vibaya kwa lengo la kujinufaisha kwa njia ambazo sio sahihi njia hizo ni pamoja na ulaghai unaoweza kusababisha utapeli mtandaoni,”amesema.
Hata hivyo amesema kuwa imebainika watumiaji wa mtandao kwa kiasi kikubwa wanachangia kufanikisha matukio mengi yanayohatarisha usalama wao mtandaoni ambapo hiyo inatokana na uelewa mdogo wa matumizi sahihi ya Tehama au kutokuzingatia kanuni za kiusalama.
“Ipo haja ya kuendelea kutoa elimu endelevu ya matumizi bora na salama ya Tehama na mtandao ili kuepusha athari za kiusalama suala matumizi sahihi na salama ya mtandaoni ni jukumu la kila mmoja wetu,”amesema.
Akitoa neno kuhusu usalama mtandaoni Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Joshua Mwangasa ameomba ushirikiano kutoka wadau na wananchi pale wanatekuwa wanatekeleza majukumu yao ya ulinzi wa mtandao kwani wao kama jeshi la polisi hawawezi kufanikiwa kwenye mapambano yao pasipo kuwa na ushirikiano wao.
Siku ya usalama mtandaoni duniani huadhimishwa Jumanne ya pili ya mwezi Februari kila mwaka ambapo ni mpango wa kimataifa ulionzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kuhamasisha matumizi sahihi na salam ya mtandao wa internet.