Farida Mangube
Katika kuadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana Katika sayansi, wasichana wametakiwa kutokuogopa kusoma masomo ya sayansi Kwa kuhofia kufanya vibaya na kushindwa kufikia malengo yao
Wito huo umetokewa na Wanafunzi wasichana kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wanaosoma fani mbalimbali, wamesema Masoma ya sayansi ni masomo kama yalivyo masomo mengine wanachitakiwa kufanya ni kusoma Kwa bidiii Ili kufikia malengo yao waliojiwekea.
Recho Mkwizu mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Shahada ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia amesema awali alipata wakati mgumu kuamua kusoma masomo ya sayansi kwani wazazi walikuwa hawaamini lakini tangia kuanza kusoma amekuwa akifanya vizuri.
“Tumekuwa tukifikiri hatuwezi jambo ambalo linaanza kwa ndugu lakini ukifika hapa SUA ukakutana na wengine wanasoma unaona ni jambo
Kwa upande wake, Catherine Sanga ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Shahada ya Familia na Sayansi za Mlaji amesema kwamba kama kutakuwa na washauri wazuri kwenye maamuzi ya kuchagua vitu vya kusomea kuanzia mwanzo kungekuwa na wimbi sawa katika masomo ya sayansi.
Kuhusu maadhimisho ya mwaka huu, Catherine amesema ni muhimu kwani yanaendelea kuwahamasisha wasichana kusomea masomo ya fani ya sayansi ili takwimu ziendana na wanaume katika usawa wa kijinsia.
Kila mwaka, Tanzania huungana na Dunia kwenye kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi ili kutengeneza usawa wa kijinsia katika fani ya teknolojia, fizikia, hesabu na uhandisi.