Na Prisca Libaga Kilimanjaro
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini tarehe 11.02.2025 imeendelea kutoa elimu kinga kwa wanafunzi juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya wilayani Same mkoani Kilimanjaro.
Aidha, Mamlaka ilimtembelea Mkuu wa Wilaya ya Same pamoja na hilo ilitembelea nyumba za upataji nafuu za Brother of Good Shepherd na Surrender for Freedom Treatment Center na jumla ya wanafunzi zaidi ya 2300 walipatiwa elimu kinga wa Shule za Sekondari za Mighareni, Angela Kairuki na Kibacha na Shule za Msingi Majevu, Kisima, pia zoezi la upandaji miti liliendelea kufanyika katika shule hizo.
DCEA Kanda ya Kaskazini iliwahamasisha wanafunzi wa Wilaya ya Same washirikiane na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya waliopo katika maeneo yao wanayoishi kupitia kupiga namba ya simu ya bure ya 119.





