Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya wazawa inayojihusisha na utoaji wa mafunzo kwa wataalamu wa TEHAMA(CYBERGEN) na watoaji wa ushauri katika mambo ya usalama mtandaoni (digital public infrastructure (DPI) ,Upendo John Kimbe akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya wazawa inayojihusisha na utoaji wa mafunzo kwa wataalamu wa TEHAMA(CYBERGEN) na watoaji wa ushauri katika mambo ya usalama mtandaoni (digital public infrastructure (DPI) ,Upendo John Kimbe amesema kuwa ,kampuni hiyo inasaidia serikali katika kufikia malengo ya utoaji huduma mbalimbali kwa wananchi kupitia serikali mtandao.
Ameyasema hayo leo mkoani Arusha wakati akozungumza na waandishi wa hahari katika kikao.kazi cha serikali mtandao (e-GA) kinachoendelea mkoani Arusha .
Amesema kuwa ,lengo la ushiriki wao kwenye kikao kazi hicho ni kuwafanya wataalamu.mbalimbali waweze kutambua kuwa kuna kampuni ya kitanzania ina uwezo wa kuleta wataalamu kutoka nje ya nchi ikiwemo Ulaya,India na Marekani.
“Tumekuja katika.kongamano hili kwa lengo la kuisaidia serikali katika kutoa huduma kwa wananchi wake kwa hiyo katika hili tumekuja katika eneo hilo la digital Tanzania kusaidia na kuona ni jinsi gani Cybergen inaweza ikachangia katika mchakato mzima wa kuifanya Tanzania kuwa ya kidigitali. “amesema Upendo .
Upendo ameongeza kuwa, kampuni hiyo imekuwa ikijihusisha na utoaji wa mafunzo ya ICT ambazo ni kozi za kitaalamu katika upande wa IT ambazo ni miongoni mwa huduma wanazozitoa ambapo wana uwezo wa kutoa huduma zote kwani wakufunzi wao wanatokea nchi mbalimbali duniani ili kuweza kuleta ujuzi wao hapa nchini .
“Katika kufanya Tanzania kuwa ya kidigitali tumeweza kuwajengea uwezo watalaamu wetu wa ndani na sio kutegemea wataalamu kutoka nje kwani ni lazima kuwajengea uwezo watu wetu wa ndani ili kuwa na Tanzania tunayoitaka.”amesema Upendo.
Aidha Upendo amewataka wadau mbalimbali kuitumia kampuni.hiyo kwa ajili.ya maswala mbalimbali ya maendeleo kwani wamekuwa wakitumia wataalamu kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuweza kubadilishana uwezo na kupata utaalamu zaidi kutoka kwa wenzetu wa nje ya nchi .
Kwa upande wake Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora , George Simbachawene akizungumza kwenye kikao kazi hicho amesema kuwa e-GA ni kiunganishi cha kupeleka huduma kwa wananchi kwa urahisi ili wananchi wapate huduma stahiki kwa haraka bila kuwepo kwa vitendo vya rushwa.
“Dunia ya leo e-GA ni kama muundo wa kurahisisha mifumo ndani ya serikali na utoaji huduma kwa urahisi katika mifumo ya serikali ,niwapongeze kwa hatua na malengo haya na mimi.kama kiongozi naridhika kuwa e-GA mmefanya kazi yenu sawasawa.” amesema Simbachawene.
Ameongeza kuwa lengo la kuandaa kikao kazi hicho ni kiwakutanisha wadau wa serikali mtandao katika.taasisi na mashirika ya umma na sekta binafsi ili kuwapatia fursa ya kujadili hatua iliyofikia katika utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao.
Naye Mkurugenzi mkuu wa e-GA ,Mhandisi Benedict Ndomba amewashukuru washiriki wote kwa kuweza kufika kwani mkutano huo utaleta tija kwao katika utendaji kazi wa kila.siku pamoja na kufanya maboresho ya mifumo ya e-GA.