Wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Njombe wametoa zawadi ya mahitaji ya kibinadamu zikiwemo taulo za kike,mafuta ya kupaka,sabuni na pampasi kwa akina mama waliyojifungua katika hospitali ya mji wa Njombe Kibena huku lengo likiwa kuwapongeza kwa jitihada walizofanya za kupigania maisha yao na watoto wao katika kipindi cha kujifungua ambacho kimekatisha maisha ya wengi duniani.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo ambae wameutaja kuwa ni zawadi akina mama hao afisa mahusiano Njombe Andrew Nyange amesema utasaidia kupunguza gharama za malezi ya watoto ambao wamewapata katika siku ya wapendanao.
Nae Regina Kavishe ambae ni Meneja wa huduma kwa wateja NMB tawi la Njombe amesema wameguswa kutambua tahamani ya mama na kisha kutembelea wodi la akina mama ili kuwapa hongera na zawadi ya kuvuka kipindi kigumu cha uzazi .
Mbali na kutoa zawadi wafanyakazi wa NMB wakiwa katika chumba maalumu cha kuhifadhi watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) wamepokea changamoto ya AC kwa ajili joto huku
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mji Kibena Dr Ayoub mturo ameishukuru benki hiyo kwa kuwapa msaada huo na kisha kueleza kwamba kuamkia februari 14 ambayo ni siku ya wapendanao watoto watano wamezaliwa hospitalini hapo huku pia akiweka wazi mahitaji makubwa ya AC katika chumba cha watoto njiti.
Nao baadhi ya akina mama ambao wamejifungua na kisha kunufaika na msaada huo akiwemo Agnes Mwalongo wanasema zawadi hizo zimekuja wakati sahihi na zitapunguza gharama za mahitaji hospitalini hapo na kisha kushuru watoaji kuguswa kiwasaidia.




