………
Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi tarehe 15.02.2025 jijini Arusha imejumuika pamoja na Wadau wa Mamlaka na Waraibu wa dawa za kulevya kusheherekea Sikukuu ya Wapendanao Duniani katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mgeni rasmi katika Sherehe hizo alikuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD) SSP. Georgina Matagi ambapo katika hotuba yake aliiomba jamii kutowanyanyapaa waraibu wa dawa za kulevya na badala yake inatakiwa kuendelea kuwapenda, kuwaheshimu, kuwathamini, kuwajali na kuwawezesha kufikia malengo yao kwani uraibu ni ugonjwa na unatibika.
Washiriki wa Sherehe hizo zaidi ya 120 walihamasishwa kuendelea kushirikiana na Mamlaka katika mapamabano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kuendelea kutoa taarifa za wahalifu wa dawa hizo katika maeneo yao wanayoishi kwa kupiga namba ya bure 119.





