Wananchi wa mkoa wa Mwanza wameendelea kujitokeza na kupata huduma kwenye Kliniki ya Sheria inayofanyika kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamati ya Ushauri wa Kisheria ya mkoa wa Mwanza.
Kliniki hiyo imeanza tarehe 17 na inaendelea hadi tarehe 23 Februari, 2025 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.