Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro ameshtakiwa na waendesha mashtaka kwa madai ya njama ya mapinduzi ya kumtilia sumu mrithi wake.
Katika jaribio la kusalia madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa 2022, mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia alidaiwa kuhusika katika mpango wa kumuwekea sumu Rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva,na kumpiga risasi Jaji wa Mahakama ya Juu Alexandre de Moraes, adui wa rais huyo wa zamani.
Mwendesha mashtaka mkuu wa Brazil Paulo Gonet Jumanne alimshtaki Rais wa zamani Jair Bolsonaro kwa jaribio la mapinduzi ili kusalia madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa 2022, katika njama iliyojumuisha pia mpango wa kumtia sumu mrithi wake na Rais wa sasa Luiz Inácio Lula da Silva.
Mwendesha Mashtaka Mkuu Paulo Gonet anadai kuwa Bolsonaro na wengine 33 walishiriki katika mpango wa kusalia madarakani.
“Wanachama wa shirika la uhalifu walipanga katika ikulu ya rais mpango wa kushambulia taasisi, kwa lengo la kuangusha mfumo wa mamlaka na utaratibu wa kidemokrasia, ambao ulipokea jina baya la ‘Green and Yellow Dagger,’” Gonet aliandika katika hati ya mashitaka yenye kurasa 272.
The post Rais wa zamani wa Brazil ashtakiwa kufanya njama ya kumuua kwa sumu rais alie madarakani first appeared on Millard Ayo.