Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila (wa kwanza kushoto) akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kirafiki la Korea nchini Tanzania (KOFIH) Gyeongbae Seo wakati akiwasili katika uzinduzi wa mradi wa kuboresha usawa wa upatikanaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira wenye lengo la kuimarisha afya za wananchi unaokwenda kutekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni, Ilala na Temeke uliofanyika leo Februari 17, 2025 jijini Dar es Salaam (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila akizungumza jambo wakati akizindua mradi wa kuboresha usawa wa upatikanaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira wenye lengo la kuimarisha afya za wananchi unaokwenda kutekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni, Ilala na Temeke.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Mohammed Mang’una akizungumza jambo katika uzinduzi wa mradi wa kuboresha usawa wa upatikanaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira unaokwenda kutekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni, Ilala na Temeke wenye lengo la kuimarisha afya za wananchi ambao wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya kuambukizwa.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kirafiki la Korea nchini Tanzania (KOFIH) Gyeongbae Seo akizungumza jambo katika uzinduzi wa mradi wa kuboresha usawa wa upatikanaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira unaokwenda kutekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni, Ilala na Temeke wenye lengo la kuimarisha afya za wananchi ambao wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya kuambukizwa.
Msimamizi wa Mradi wa kuboresha usawa wa upatikanaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanamvua Zuberi akizungumza jambo katika uzinduzi wa mradi huo unaokwenda kutekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni, Ilala na Temeke wenye lengo la kuimarisha afya za wananchi ambao wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya kuambukizwa.
Mwakilishi wa Wizara ya Afya Salvata Silayo akizungumza jambo katika uzinduzi wa mradi wa kuboresha usawa wa upatikanaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira unaokwenda kutekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni, Ilala na Temeke wenye lengo la kuimarisha afya za wananchi ambao wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya kuambukizwa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kirafiki la Korea nchini Tanzania (KOFIH) Gyeongbae Seo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Mohammed Mang’una, Mwakilishi wa Wizara ya Afya Salvata Silayo ,Msimamizi wa Mradi wa kuboresha usawa wa upatikanaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanamvua Zuberi pamoja na wataalamu wa afya kutoka Manispaa ya Kinondoni, Ilala na Temeke wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha za matukio mbalimbali
………..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila amezindua utekelezaji wa mradi wa kuboresha usawa wa upatikanaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira wenye lengo la kuimarisha afya za wananchi ambao wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya kuambukizwa, huku akiwataka wasimamizi wa mradi huo kufanya kazi kwa bidii na ufanisi.
Mradi huo unatekelezwa katika Manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke kwa ushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kirafiki la Korea (KOFIH) ambao wamefadhili shilingi bilioni 1.75 ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi na kuleta tija.
Akizungumza leo Februari 17, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizindua mradi huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila, amesema kuwa mradi unakwenda kufanya kazi katika Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuokoa maisha ya wananchi ambao wanaishi katika mazingira hatarishi ya kupata magonjwa ya kuambukizwa.
Dkt. Nguvila amesema kuwa mradi huo unakwenda kupambana na magonjwa ya homa ya dengue, Malaria, kipindupindu, kununua mashine za kupima magonjwa ya kuambukizwa, kuboresha maabara za vituo vya afya pamoja na kuongeza uwelewa kwa wataalamu wa afya.
“Watendaji tunataka kuona ufanisi na tija kwa faida ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kuokoa maisha, tujitume na kusimamia kwa uweledi ili kufikia malengo na kupata matokeo chanya” amesema Dkt. Nguvila.
Mwakilishi wa KOFIH nchini Tanzania Gyeongbae Seo, amesisitiza umuhimu wa mradi katika kutokomeza magonjwa kwa wananchi, huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa mradi yenye lengo kuisaidia jamii.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Mohammed Mang’una, amesema kuwa mradi huo pia unakwenda kutokomeza magonjwa yanayotokana na uchafu ikiwemo mifumo ya maji ambayo sio safi na salama, huku akifafanua kuwa matokeo ya mradi yakiwa mazuri wataingia awamu ya pili kwa kuzifikia halmashauri nyengine.
Dkt. Mang’una, amesema kuwa mradi umelenga kuzigusa Kata zenye watu wengi pamoja na changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya ikiwemo miundombinu kwa lengo la kuwakinga na milipuko wa magonjwa ya kuambukizwa.
Mwakilishi wa Wizara ya Afya Salvata Silayo amelishukuru Shirika la Maendeleo la Kirafiki la Korea (KOFIH) kwa kufadhili mradi huo, huku akisisitiza umuhimu kwa watendaji katika kuhakikisha malengo husika yanafikiwa na kuleta tija.
Nae, Msimamizi wa Mradi wa kuboresha usawa wa upatikanaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira Mkoa wa Dar es Salaam Mwanamvua Zuberi, amesema kuwa mradi huo utadumu kwa muda wa miaka mitano ambapo unakwenda kufanya kazi kwa wananchi hasa wanaoishi katika makazi ambayo sio rafiki.
Katika uzinduzi huo wataalamu wa Afya pamoja na timu kutoka KOFIH walijadiliana kuhusu mikakati bora ya kutekeleza mradi huo kwa ajili ya kuboresha huduma za afya pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za msingi kwa jamii.