Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis leo tarehe 25 Februari, 2025 Makongo Juu jijini Dar es Salaam
akisaini kitabu cha maombolezo katika msiba wa Marehemu Bi. Sifael Mushi,
aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa Muunganio wa Tanganyika na
Zanzibar, ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis leo tarehe 25 Februari, 2025 Makongo Juu jijini Dar es Salaam
akitoa heshima ya mwisho kwa mwili wa Marehemu Bi. Sifael aliyeshiriki tukio
la kuchanganya udongo wa Muunganio wa Tanganyika na Zanzibar, ambaye
amefariki dunia Februari 20, 2025.
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah
Hassan Mitawi leo tarehe 25 Februari, 2025 Makongo Juu jijini Dar es Salaam
akitoa heshima ya mwisho kwa mwili wa Marehemu Bi. Sifael aliyeshiriki tukio
la kuchanganya udongo wa Muunganio wa Tanganyika na Zanzibar, ambaye
amefariki dunia Februari 20, 2025.
…………….
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis leo tarehe 25 Februari, 2025 Makongo Juu jijini Dar es Salaam
ameungana na viongozi na waombolezaji katika kuifariji familia ya Marehemu
Bi. Sifael Mushi, aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa Muunganio wa
Tanganyika na Zanzibar, ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Marehemu Bi. Sifael amefariki dunia katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es
Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Akitoa salamu za Serikali mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili
wa Marehemu Bi. Sifael, Naibu Waziri Khamis amesema marehemu amefanya
kazi kubwa kwa taifa kwa kuweka historia ya Muungano ambao hadi leo
matunda yake yanaonekana.
Mhe. Khamis amesema Marehemu Sifael alikuwa mtu wa watu na mmoja wa
watu muhimu katik taifa hili aliyetengeeza historia kubwa ambayo itakwenda
kudumu milele hata kizazi kinachokuja kitakwenda kutambua mchango wake.
“Leo hii tunaona Muungano wetu ulivyo imara na unaendelea kudumu na hata
wananchi wa pande zote mbili wanashirikiana, wanavuka maji (bahari) kutoka
upande mmoja kwenda mwingine yote ni kwasababu ya kazi kubwa
aliyoifanya mama huyu,” ameeleza.
Mhe. Naibu Waziri ametumia nafasi hiyo Mhe. kuwasilisha salamu rambirambi
kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. Philip Mpango
Amesema viongozi hao wakuu wapo pamoja na familia ya marehemu na
wanatoa pole kwa kumpoteza mtu muhimu katika taifa hili na kwamba
ataendelea kukumbukwa na kusomwa katika historia.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule
aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema
kizazi cha sasa kina mengi ya kutafakari na kujifunza kutokana na maisha ya
viongozi walioasisi Muungano ambao unatimiza miaka Zaidi ya 60.
Amemtaja Marehemu Sifael kuwa ni mfano wa kuigwa kwa kazi ya uzalendo
na utii aliounesha alipokuwa miongoni mwa Watanzania walioshiriki katika
zoezi la kuchanganya udongo wa Muungano.
Hivyo, Mkuu wa Wilaya amesema kuwa Watanzania wana jukumu kubwa la
kumshukuru Mungu na kuiombea roho ya marehemu apate pumziko la amani.
Naye Msemaji wa familia Bw. Rwegasha ameishukuru Serikali ya Rais Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa upendo
waliouonesha kwa familia.
Mwili wa Marehemu Sifael umesafirishwa Machame wilayani Hai Mkoa wa
Kilimanjaro na unatarajiwa kupumzishwa tarehe 26 Februari, 2025.
Katika shughuli hiyo Mhe. Naibu Waziri aliambatana na Naibu Katibu Mkuu
(Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi na
wataalamu mbalimbali kutoka Ofisi hiyo.
Marehemu Sifael alikuwa ni miongoni mwa vijana wa Kitanzania wanne
walioshiriki katika tukio la kuchanganga udongo wa iliyokuwa Tanganyika na
Zanzibar, tarehe 26 Aprili, 1965 wakati wa sherehe za mwaka mmja wa
Muungan uliosasisiwa tarehe 26 Aprili, 1964.
Wengine walioshiriki katika tukio hilo na wametangulia mbele ya haki ni
Marehemu Hassanieli Mrema aliyefariki Mei 04, 2024, Marehemu Khadija
Abbas Rashid alifariki Agosti 22, 2023 na Marehemu Omar Hassan Mkele
alifariki Agosti 28, 2024.