Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis amesema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi wakati wa
Ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Bi. Sifaeli Mushi, aliyeshiriki tukio la
kuchanganya udongo wa Muungano iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Machame wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro leo
tarehe 26 Februari, 2025. Marehemu Bi. Sifael ambaye alifariki dunia tarehe 20 Februari, 2025 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis akiwa na viongozi mbalimbali akishiriki Ibada ya kuuaga mwili
wa Marehemu Bi. Sifaeli Mushi, aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa
Muungano iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Machame wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro leo tarehe 26 Februari, 2025.
Marehemu Bi. Sifael ambaye alifariki dunia tarehe 20 Februari, 2025 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis akiweka shada la maua wakati wa maziko ya mwili wa
Marehemu Bi. Sifaeli Mushi, aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa
Muungano, mara baada ya ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Machame wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro leo
tarehe 26 Februari, 2025. Marehemu Bi. Sifael ambaye alifariki dunia tarehe
20 Februari, 2025 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis akikabidhi picha yenye taswira ya tukio la kuchanganya
udongo wa Muungano kwa mwanafamilia ya Marehemu Bi. Sifaeli Mushi,
ambaye alishiriki tukio hilo, mara baada ya maziko nyumbani kwa marehemu
Machame wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro leo tarehe 26 Februari, 2025.
Marehemu Bi. Sifael ambaye alifariki dunia tarehe 20 Februari, 2025 jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais
Bi. Christina Mndeme na katikati ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanznaia (KKKT) Frederick Shoo.
………….
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imesema inatambua na kuthamini
mchango wa walioshiriki katika kuasisi na kuudumisha Muungano hususan wakati
tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis amesema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi wakati wa
Ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Bi. Sifaeli Mushi, aliyeshiriki tukio la
kuchanganya udongo wa Muungano iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Machame wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro leo tarehe
26 Februari, 2025. Marehemu Bi. Sifael ambaye alifariki dunia tarehe 20
Februari, 2025 jijini Dar es Salaam.
Mhe. Khamis, alikuwa mzalendo ambaye hakusita wakati wote kueleza mazuri
yote na faida za Muungano huu adhimu hususan kwa vijana ili kuulinda na
kuutetea.
“Bi. Sifaeli alikuwa ni mmoja wa vijana walioshiriki tukio la kuchanganya udongo
wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika tarehe 26 Aprili, 1965 katika sherehe za
mwaka mmoja wa Muungano zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es
Salaam. Alishiriki katika tukio hilo akiwa kijana mwenye umri wa miaka 32
pamoja na wenzake watatu (Mzee Hassan Omari Mzee kutoka Zanzibar, Bi.
Khadija Abasi Rashid kutoka Zanzibar na Bw. Hasanieli Elisaeli Mrema kutoka
Tanzania Bara),“ amesema Naibu Waziri.
Amesema kwa kutambua mchango huo, Ofisi ya Makamu wa Rais pia iliwahi
kuwaalika wazee hao Bungeni wakati wa kusoma hotuba ya bajeti ya Ofisi ya
Makamu wa Rais tarehe 3 Mei, 2016 na walishiriki ambapo tukio la mwisho
ambalo alishiriki na wenzake watatu ni Maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano
katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma tarehe 26 Aprili, 2018, tukio hili aliweza
kushiriki na wenzake wote watatu.
Halikadhalika, Mhe. Khamis amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa
wazee hao wanne ambao wote ni marehemu, hivyo mwaka 2014 walitunukiwa
Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja la Nne. Nishani hizi
zilitolewa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano,
Awamu ya Nne katika Hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 26 Aprili,
2014.
Aidha, Naibu Waziri amewaasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na salamu kutoka wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Akitoa salamu zake Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT Frederick Shoo
ambaye aliongoza ibada ya kumuaga Marehemu Sifael aliwataka Watanzania
kuwekeza katika elimu.
Alisema ni muhimu kuiga mazuri ya marehemu hususan katika suala la elimu
ambalo aliitumikia kwa moyo wote katika kipindi cha uhai wake wakati
anafundisha wanafunzi.
Mara baada ya ibada hiyo mwili wa Marehemu ulipelelekwa nyumbani kwake kwa
ajili ya maziko ambayo yalihudhuriwa na ndugu, jamaa na wananchi mbalimbali
umezikwa nyumbani kwake Machame