Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akichangia mada wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo akiwa katika kazi ya vikundi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dr. Maulid Maulid akielezea malengo ya Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo (kulia) akizungumza jambo na Kiongozi wa Timu (Shule Bora) Bi. Virginie Briand (kushoto) na Bi. Zainab Dhanani (katikati) kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dr. Maulid Maulid akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera,Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo.
Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam
Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Idara ya Uendelezaji Sera, Bi. Mwanaamani Mtoo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya jitihada kubwa katika kuwawezesha wanawake kupiga hatua kimaendeleo.
Bi. Mtoo ameyasema hayo leo kwenye Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililolenga kujadili kuhusu Wanawake na Uongozi katika Elimu lililofanyika Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya WhiteSands jijini Dar es Salaam.
Amesema uwezeshwaji wa wanawake umefanyika kwa ushirikiano wa Viongozi wa Serikali pamoja na wanawake na wanaume kwani hakuna maendeleo ya wanawake pasipokuwa na wanaume kama ambavyo Sera ya Menejimenti na Ajira ya Mwaka 2008 ilivyotanabaisha katika Sura ya 5 ambayo inazungumzia Anuai za Jamii katika Utumishi wa Umma ambao umeleta msukumo mpya wa ufanisi na tija kwenye utendaji kazi kwa kutumia ujuzi na vipaji walivyonavyo.
Aidha, Bi. Mtoo amesema kwenye Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 298 pamoja na Kanuni za Mwaka 2022 zimeelekeza uzingatiaji wa masuala ya kijinsia ambapo Ofisi hiyo imetoa Mwongozo wa Ujumuishwaji wa Jinsia unaopaswa kutumika wakati wa usimamizi wa rasilimaliwatu ikiwemo kwenye masuala ya usaili na michakato ya ajira ili kuhakikisha watumishi wanawake au kundi la jinsi yenye uwakilishi mdogo linapewa fursa katika nafasi za ajira kwa kuzingatia sifa na vigezo.
“Mwongozo huu ni kielelezo tosha cha dhamira ya Serikali ya kuimarisha ujumuishwaji wa jinsia katika Utumishi wa Umma jambo ambalo ni muhimu katika kuboresha utendaji kazi serikalini unaoiwezesha Serikali kuimarisha uchumi wa nchi na utoaji wa huduma kwa wananchi wote.” Amesisitiza Bi. Mtoo.
Ameipongeza Wizara ya Elimu kwa kuleta mapinduzi kwenye Sekta ya Elimu ambayo kwa kiasi kikubwa imewezesha kuibua viongozi mbalimbali wakiwemo wanawake kujumuishwa na kuleta uwiano sawa wa jinsia.
Ameongeza kuwa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kutambua thamani ya mwanamke, inampongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo katika taifa hili.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid Maulid amesema kongamano hilo limelenga kujadili mustakabali wa Mwanamke na Uongozi katika Elimu ambapo itawawezesha kupata maoni, ushauri na mapendekezo yatakayoleta matokeo na mikakati itakayowezesha kupiga hatua kubwa kwa maendeleo ya ustawi wa taifa.