Na Mwandishi Wetu

Elimu hii imetolewa kuanzia Machi 10 hadi 12, 2025, katika mikoa ya Lindi, Pwani, Mbeya, Songwe, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Manyara na Kigoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.
FCC inalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu haki zao kama walaji, namna ya kushughulikia malalamiko dhidi ya huduma duni au bidhaa zisizokidhi viwango, pamoja na usimamizi wa mikataba ya mlaji inayotolewa na watoa huduma mbalimbali.
Aidha, wananchi wanapata fursa ya kuwasilisha malalamiko yao moja kwa moja kwa Tume ya Ushindani (FCC) ili kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani.
Tume imeeleza kuwa elimu hiyo ni muhimu kwa walaji na wafanyabiashara ili kuhakikisha biashara zinaendeshwa kwa ushindani wa haki na walaji wanalindwa dhidi ya mbinu kandamizi.
Pamoja na hayo FCC pia inahimiza wananchi kutumia madawati maalum ya ushauri ili kupata msaada wa kisheria na kiuchumi wanapokumbana na changamoto katika masuala ya manunuzi na huduma.
Maadhimisho hayo yamepata usaidizi kutoka kwa mashirika kama Foundation for Civil Society (FCS) na Benki ya NMB, ambayo yamechangia kufanikisha utoaji wa elimu kwa jamii.
Watumishi wa Tume ya Ushindani (FCC) wakiwanafanya kiliniki ya kutoa elimu kwa wanachi Ruangwa mkoa wa Lindi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani..jpeg)
.jpeg)
Timu ya watumishi wa FCC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakitoa elimu kwa wafanyabiasha katika standi ya Mlowo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.