Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina inatarajia kufanya mkutano na wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache, takribani 150 kutoka kampuni 56, kuanzia Machi 25-28, 2025.
Kaulimbiu ya Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 25 hadi Machi 28, 2025 katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha, Pwani ni ‘Matumizi ya Teknolojia katika Kuboresha Utendaji’.
Mkutano huu unalenga kutoa nafasi ya majadiliano kuhusu mchango wa teknolojia linapokuja suala la maamuzi yatokanayo na data “data-driven decision making” na ufanisi wa taasisi.
Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.