Na. Josephine Majura WF, Mara
Serikali inatambua umuhimu wa kuhakikisha kwamba makundi yote maalumu, yakiwemo watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi), wanawake, vijana, na wazee, wanapata elimu ya fedha nchini ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Hayo yameelezwa na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya , wakati wa mafunzo kwa watu wenye ulemavu wa kusikia yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
“Elimu hii inalenga kuyawezesha makundi haya kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi, kuwajenga uwezo wa kusimamia rasilimali zao, na kuboresha maisha yao kwa ujumla”, alisema Bw. Kibakaya.
Alisema kuwa katika utoaji wa elimu ya fedha katika makundi mbalimbali nchini, washiriki wamepewa elimu katika maeneo ya usimamizi wa fedha binafsi, uwekaji akiba, mikopo, uwekezaji, bima, bima ya amana, kodi na kujipanga kwa maisha ya uzeeni.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Bw. Athuman Khalid (mlemavu wakusikia) alieleza furaha yake kwa kupata fursa ya kushiriki mafunzo ya elimu ya fedha.
“Kwa muda mrefu tulihisi kutengwa katika masuala ya fedha, lakini leo tumefikiwa na kupewa elimu kuhusu kupanga matumizi, kujiwekea akiba, kufanya uwekezaji na kutumia Taasisi rasmi kuchukua mikopo”, alisema Bw. Khalid.
Naye Mkalimani, Bi. Dainess Wilson, aliiomba Serikali kuendelea kutoa mafunzo endelevu kwa Wakalimani nchini ili kuboresha ujuzi na weledi wao katika kazi na kutoa huduma za utaalamu wa hali ya juu na kuongeza tija katika utendaji wao.
Wizara ya Fedha kwa kutambua umuhimu wa mchango wa Taasisi za Fedha Timu ya Wataalamu kutoka wizarani ambayo ipo mkoani Mara kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali imeambatana na Wataalamu kutoka Taasisi nyingine za Serikali, ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS na NSSF, pamoja na Taasisi za Kibenki ikiwemo, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Benki ya Biashara Tanzania (TCB), CRDB, NMB, NBC.
Mkazi wa Manispaa ya Musoma, Bw. Athuman Khalid (mlemavu wa kusikia) akiishukuru Serikali kwa kuwafikia kundi la wasiosikia kuwapa elimu ya masuala ya fedha kwa kuwa itawakomboa kiuchumi wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara, katika picha hiyo yupo pia Mkalimani Bi. Dainess Wilson, akitafsiri lugha ya alama.
Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mzava (kulia) na Afisa Mahusiano wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), wakimkabidhi zawadi ya fulana, Bi. Catheline Philipo, baada ya kujibu swali kuhusu maeneo salama ya kutunza fedha wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bw. Stanley Kibakaya, akitoa elimu kwa Bi. Juliana John kwa njia ya kipeperushi ambacho kina taarifa mbalimbali kuhusu uwekaji akiba, wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Mkalimani, Bi. Dainess Wilson, akitafsiri lugha ya alama mafunzo ya elimu ya fedha kwa kundi la watu wenye ulemavu wa kusikia walioshiriki mafunzo hayo yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC l, yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Baadhi ya watoa huduma katika Taasisi za Fedha ikiwemo Benki ya NMB, CRDB, TCB, NBC pamoja na NSSF wakifuatilia mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha, kundi maalumu la watu wenye ulemavu wa kusikia wakifuatilia elimu iliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF, Benki Kuu ya Tanznaia (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Mara)