Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kupokea majina ya wagombea watano (5) wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo kwa Kanda ya Afrika akiwemo pia Prof. Mohamed Janabi ambaye anaiwakilisha Tanzania.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya WHO Machi 14, 2025 inaeleza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Duniani Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amepokea majina ya wagombea hao kutoka nchi wanachama wa WHO Kanda ya Afrika.
Prof. Janabi atachuana na Dkt N’da Konan Michel Yao kutoka Côte d’Ivoire, Dkt. Dramé Mohammed Lamine kutoka Guinea, Dkt. Boureima Hama Sambo kutoka Niger pamoja na Prof. Mijiyawa Moustafa kutoka Togo.
WHO itaendesha tena uchaguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika hivi karibuni, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika hilo Dkt. Faustine Ndungulile kilichotokea Novemba 27, 2024.
Fuatilia kurasa zetu kwa habari zaidi za uchaguzi huu.