NA DENIS MLOWE, IRINGA
Aidha, kamati hiyo imeiagiza halmashuri hiyo kutoa taarifa inayojitosheleza ambayo itaeleza kwa kina kuhusu mradi huo (Business Plan) kwa wizara ya Tamisemi ili kuleta ushawishi mapema kujua changamoto na kama kuna matatizo ieleze ni nani alisababisha hilo na hatua gani zimechukuliwa kuweza kuwezesha mradi huo kufanya kazi na kuleta faida kwa jamii.
Akiwasilisha maagizo hayo, kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati Halima Mdee ,Mjumbe wa kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi, Omary Kiguo alisema kuwa maagizo licha ya kutoa hadi disemba 30 mwaka huu kuhakikisha wanakamilisha machinjio hayo pia wametoa maagizo katika maeneo ya mengine mawili kuweza kukamilika kwa wakati yaweze kuhudumia wananchi.
Alisema kuwa baada ya kufanya ziara katika maeneo hayo wametoa agizo kuhakikisha kwamba afisa masuhuri ahakikishe taratibu za kisheria zinafatwa katika kukata kiasi cha milioni 18.6 zinazotakana na ucheleweshaji uliofanywa na Mkandarasi Ngogo Engeneering .
Aidha kamati iliagiza kwamba Afisa Masuhuri kuhakikisha kwamba wanakamilisha mradi huo hadi Disemba 30 mwaka 2027 na taarifa ya kila nusu mwaka ya ukamilishaji wa mradi uwasilishwe kwa CAG kwa ajili ya uhakiki.
Kamati iliongeza kuwa afisa masuhuri afanye upembuzi yakinifu ,sanifu na tathmini ya kina namna ya mradi wa machinjio ya kisasa ya Ngelewala utaonyesha gharama halisi za ukamilishaji wa mradi na muda ambao utakamilika na kuanza kutoa huduma ili kuepukana na ongezeko la mawanda na gharama za mradi na taarifa hiyo iwasilishwe kwa CAG kwa ajli ya uhakiki kabla ya tarehe 30 Juni 2025.
Kamati ilisema kuwa afisa masuhuri aandae mpango mkakati pamoja mpango wa biashara kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji wa mradi huo ukijumuisha muda ambao gharama za mradi zitarejeshwa na faida ambayo itatokana na mradi wa machinjia ya kisasa na kuwasilisha kwa CAG kabla ya tarehe 30 Julai 2025.
Kwa upande wake Mkurgenzi wa Manispaa ya Iringa,Justis Kijazi alisema kuwa mradi wa Ngelewala waliandikia andiko ukaingia katika miradi ya kimkakati hivyo maagizo yote ambayo kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeiagiza watafanyia kazi .
Alisema awali mkandarasi wa mradi huo aliwazungusha hivyo halmashauri ikachukua hatua za kuchukua certificate yake iliyoitoa wakakata kiasi cha fedha kinachotakiwa lengo ikiwa ni kumwonyesha kwamba asipokuja kuendelea na mkataba wake hatua zaidi zitachukuliwa.
Alisema kuwa halmashauri hiyo inahitaji kiasi cha bilioni 1.9 kuweza kukamilisha mradi huo kwa kuweka vifaa vya kisasa vya machinjio kuliko vilivyopo sasa hivi
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Festo Dugange,alisema kuwa maelekezo ambayo kamati imetoa kazi ya wizara ni kuyafanyia kazi ili yaweze kufikia viwango vinavyokubalika na yaweze kutoa huduma kwa wananchi kama mipango ilivyopangwa.
Alisema kuwa ni dhamira ya serikali na Rais wa Tanzania ,Dr.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba miradi yote na fedha zote zinazoletwa kwenye halmashauri zinatumika kadri ya mipango,kwa kuleta thamani ya fedha,ufanisi wa miradi kutoa huduma zenye tija zinazotarajiwa hivyo yale yote ambayo kamati imeigiza ni wajibu wa wizara kuyatekeleza.
“Nikuhakikishie Mh, mwenyekiti tutaendelea kuboresha kwenye mapengo na kuhakikisha kwamba tunafikisha miradi kwenye maeneo yanayotakiwa” alisema
Meya wa Manispaa ya Iringa , Ibrahimu Ngwada alisema kuwa kama halmashauri imechukua yote yaliyotolewa agizo na kamati na kuwashukuru kwa kuwapa elimu kubwa jinsi ya kujenga hoja na maswali kwa upande wao kwani kuna baadhi ya viongozi wako kwa ajili ya kufokea watu wa chini ila hawatoi elimu nini kifanyike tofauti na kamati hiyo ambayo imekuwa kama shule kwao kujifunza.