Na Beatus Maganja, Mbeya.
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA imekutana leo Machi 18, 2025 Jijini Mbeya Kwa ajili ya kuanza kikao chake cha Kawaida cha 30 cha Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis R. Semfuko.
Katika kikao cha siku ya Kwanza (Leo) wajumbe wa kamati za Sera, Mipango na Fedha inayoongozwa na Dr. Simon Mduma na kamati ya Ulinzi wa Rasilimali ya Wanyamapori na Uendeshaji na Usimamizi wa Rasilimali watu inayoongozwa na Prof. Jafari Kideghesho wamekutana na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Maendeleo na ustawi wa Taasisi hiyo.