Askari Polisi nchini wametakiwa kuendelea kuchukua hatua kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto ili kudhibiti vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara kwenye jamii.
Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Faidha Suleiman akiwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Wilfred Willa wakati akitoa mada kwa wanafunzi wa kozi ya Uafisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Machi 18,2025 huku akiwaonya baadhi ya askari Polisi kutokuwa sehemu ya kutekeleza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Akitoa mada kwa wanafunzi hao, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Wilfred Willa, amewakumbusha kuhusu wajibu wa afisa wa Polisi katika kushughulikia makosa ya ukati wa kijinsia namna sahihi ya kudhibiti vitendo hivyo kwenye jamii.
Aidha, wanafunzi hao wa kozi ya Uafisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi wamejengewa uwezo wa kutambua viashiria vya ukatili wa kijinsia, athari za vitendo hivyo, hatua za kuchukua ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo.


