Walimu 646 wa Shule za Msingi Wanufaika na Mafunzo ya mbinu za ufundishaji yanayoendeshwa na Serikali chini ya ufadhili wa Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania (BOOST).
Walimu hao ni wa shule za Msingi kutoka mikoa sita ambayo ni Dodoma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, na Ruvuma wanashiriki mafunzo yanayolenga kuboresha mbinu za ufundishaji na kuimarisha mazingira salama ya ujifunzaji kwa wanafunzi.
Mafunzo hayo yameanza Machi, 18, 2025 katika Chuo cha Ualimu Klerruu, mkoani Iringa.
Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia, pamoja na umoja wa wazazi na walimu (UWAWA).