Sheikh wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hasani Kabeke, amesema ili kukamilisha mradi wa ujenzi wa vituo vya afya zinavyohitajika sh.bilioni 4.5, jumla ya sh. milioni 100 zimetolewa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, sh. milioni 200 kutoka fedha za ndani na sh. milioni 8.9 kutoka kwa wadau.
“Hapa zinatafutwa sh.bilioni 1.5 tuendeleze mradi huu,hivyo tusitishwe na kifo iwe mvua au jua hatushindwi lazima vituo vijengwe ili hata tukiondoka tuache alama,”amesema.
Sheikh Kabeke ameomba msaada wa serikali za wilaya za Magu na Misungwi,ili kupata viwanja vya kujenga vituo vya afya huku akieleza kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe tayari amewapatia kiwanja cha kujenga kituo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa vituo saba vya afya, Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Issa Kwezi, amempongeza Sheikh Kabeke, kwa maono yake ya kipekee,ubinifu na uongozi bora, hivyo wananchi wa Mkoa wa Mwanza wanapaswa kumuunga mkono kutekeleza mradi huo.
“Sheikhe Kabeke tunakupongeza unafanya kazi kubwa,sisi Simiyu tumeiga na kujifunza kutoka Mwanza,huko nyuma hatukuwahi kuona gari la BAKWATA mtaani,sasa ujenzi vituo vya afya vinajengwa kwa ubunifu na weledi wako,unastahili pongezi,”amesema Sheikh Kwezi.
Ameongeza kuwa; “Wasukuma kuna kitu wanaita Ndhulu (choroko) hata ukizipika utakuta nyingine haijaiva,wapo watu hata uwapike vipi hawaivi, ukifanya mazuri hawayaoni hao wanaweza kukukwamisha,wakati mingine uwasamehe tu.Sisi Simiyu kwa mapenzi makubwa tutakuunga mkono kwa sh.1,000,000.”
Viongozi mbalimbali kutoka wilaya za Kigoma na Magu pia walishiriki kwa kutoa michango ya kifedha na vifaa vya ujenzi wa vituo vya afya,huku wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano na umoja katika maendeleo ya kijamii.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini,Haruna Kambilo amechangia saruji mifuko kumi,ambapo amesema anayoyafanya Sheikh Kabeke ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na anamuunga mkono Rais Samia katika maendeleo, viongozi wanafurahia na hivyo wataendelea kumuunga mkono.
Diwani wa Kitongoni (CCM) Kigoma Mjini,Himid Mkunda amechangia sh.1,000,000,akwataka waislamu kuendeleza umoja huo,kwamba kinachofanywa na BAKWATA Mwanza nchi ingekuwa mbali na vituo vya afya vinavyojengwa watatibiwa watu wa dini na imani tofauti ambapo.






