Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Kituo cha Kulea Watoto wa Mtaani cha Amani Center tarehe 18.03.2025 imetoa mafunzo maalum juu ya mbinu za kujiepusha na tatizo la dawa za kulevya kwa watoto wa mtaani 9 waliopo katika kituo cha Amani Center kilichopo Ngarenaro jijini Arusha.
Watoto hao wa mtaani ambao wapo katika hatari kubwa ya kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya walifundishwa mbinu mbalimbali za kujizuia na vishawishi vinavyoweza kuwapelekea kutumia dawa hizo.
Pia walihimizwa kushirikiana na Mamlaka kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kupitia namba ya simu ya bure ya 119 ili kuhakikisha watu wanauza dawa mitaani wanaweza kudhibitiwa kwa mujibu wa sheria.