Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele akimkabidhik adi mpya ya Mpiga Kura Ndg. Abubakari Majuto mkazi wa Mzambarauni Kata yaG ongola Mboto Dar es Salaam ambaye ni mlemavu wa viungo alijitokeza kujiandikishak atika kituo cha Shule ya Msingi Mzambarauni leo Machi 18, 2025.
Gongola Mboto Dar es Salaam ambaye ni mlemavu wa viungo alijitokeza kujiandikisha katika kituo cha Shule ya Msingi Mzambarauni leo Machi 18, 2025.
Wananchi wakiwa katika moja ya vituo Jijini Dar es Salaam kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Wapiga Kura Mkoani Dar es Salaam na kushuhudia mwenendo wa zoezi hilo katiuka siku ya pili.
Wapiga Kura Mkoani Dar es Salaam na kushuhudia mwenendo wa zoezi hilo katika siku ya pili.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, leo Machi 18, 2025, ametembelea na kukagua vituo vya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, katika Jimbo la Temeke, lililopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, leo Machi 18, 2025, ametembelea na kukagua vituo vya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, katika Jimbo la Temeke, lililopo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo tarehe 18 Machi, 2025 ametembela vituo mbalimbali vya kuandikisha Wapiga kura Jimbo la Ilala Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuona zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linavyoendelea.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo tarehe 18 Machi, 2025 ametembela vituo mbalimbali vya kuandikisha Wapiga kura Jimbo la Ilala Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuona zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linavyoendelea.
Wananchi wa Kata ya Kivule jijini Dar es Salaam wakiwa wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboiresha taarifa zao katika kituo cha Ukooni Kivule.
Na. Mwandishi Wetu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema
itaongeza mashine za BVR na watendaji katika vituo ambavyo vimebainika kuwa na
watu wengi ili kufanikisha uandikishaji na uborteshaji wa taarifa katika Daftari la Kudumu lka Wapiga Kura mkoani Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo Machi 18, 2025 katika siku ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati akikagua
vituo Mkoani Dar es Salaam.
“Leo katika siku ya pili ya zoezi
nimetembelea vituo vya uboreshaji na waliojitokeza wamekua wengi mmno kiasi kwamba vifaa vinaonekana ni vichache, nimeagiza vifaa kwamba viongezwe na vituo viongezwe ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema Mhe. Jaji wa
Rufani Mwambegele.
Jaji Mwambegele akiwa katika Kituo cha Lukooni Chanika Jijini Dar es Salaam alishuhudia uwepo wa wananchi wengi waliojitokeza
kwaajili ya kuboresha taarifa zao na kujiandikisha na kutoa maagizo ya
kuongezwa kwa mashine za BVR katika kituo hicho.
“Hapa Lukooni eneo la Chanika katika Wilaya ya Ilala kulikua na kituo kimoja katika siku ya kwanza, lakini baada ya kubaini kwamba watu wanakua ni wengi na wanatumia muda mrefu nikaagiza vifaa viongezwe na leo nimepita bado nimeona BVR mbili hazitoshi kwahiyo nimeagiza ziongezwe ili kuweza kukabiliana na changamoto hii,” aliongeza Jaji Mwambegele.
Aidha, Jaji Mwambegele amepongeza wananchi wote waliojitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika siku za mwanzo za zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu kwani kufanya hivyo
kunawezesha wao kukamilisha zoezi hilo ndani ya siku saba kama ilivyopangwa. Nae afisa Mwandikishaji wa Jiji la Dar es Salaam, Faraja Nakua amesema katika Majimbo matatu yaliyopo katika Halmashauriu
ya Jiji la Dar es Salaam yenye majimbo ya Ilala, Ukonga na Segerea zoezi
linakwenda vyema na wao wamejipanga kufanikisha zoezi hilo.
“Nizidi kuwahamasisha wananchi wa Majimbo ya Ukonga, Ilala na Segerea Jijini Dar es Salaam kuendelea kujitokeza kwa wingi na sisi tumejipanga kutekeleza zoezi hili kama ambavyo Tume imeagiza na vifaa tulivyotakiwa kuongeza vipo tutavipeleka katika maeneo yote yenye changamoto,”
alisema Nakua.
Nae Atness Shayo mkazi wa Ukonga Mzambarauni na Hassan Said Mmanga wa Chanika wamepongeza ujio wa zoezi hilo kwani walipoteza kadi zao za mpiga Kura na sasa wameoata kadi zao mpya zitakazoweawezesha kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu baadae mwaka huu.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inataraji kuandikisha Wapiga Kura wapya 643,420 mkoani Dar es Salaam ambapo jumla ya vituo 1,757 vinatumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 96 katika vituo 1,661 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.
Aidha Tume imejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wote wenye sifa za kuandikishwa wanaandikishwa kwani BVR zaidi ya 5,000 na watendaji wa kutosha wapo kwaajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.
Tume imeshakamilisha uboreshaji wa Daftari katika Mikoa 29. Kwa mujibu wa ratiba, leo Tume inaanza uboreshaji katika mzunguko
wa 13 ambao ni mzunguko wa mwisho wa uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu unahusisha Mkoa wa Dar es Salaam pekee.
Kailima amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 643,420 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 3,427,917 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na wapiga kura 4,071,337 idadi ambayo inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa
uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au nyingine
hawakuweza kujiandikisha.
Zoezi la uboreshaji wa Daftari linahusu kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka
2025, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine.
Uboreshaji wa Daftari pia unahusu kutoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye Daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa
ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania na kifo.