Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Prosper Mgaya, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa chuo hicho katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Machi 20, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.

Dkt.Mgaya, amesema Serikali imenunua ndege mbili za mafunzo aina ya Cesna 172 zenye injini moja ambazo tayari zipo nchini kwaajili ya kuanza mafunzo hayo.
“Ndege hizi zina thamani bil 2.9 na serikali ipo katika taratibu za ununuzi wa ndege nyingine tatu ikiwa ndege moja ya injini mbili ambayo itawasili mwezi Oktoba 2025 ambayo ina thamani ya bil.5.9, na Ndege mbili za injini moja zitawasili mwaka 2026.”amesema