Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, tarehe 20 Machi 2025, jijini Dar es Salaam. amekutana na kuwa na mazungumzo na Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Utalii wa Japan Onodera Seiich ambae yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika mafunzo ya fani mbalimbali za ujuzi.
Katika mazungumzo hayo,Prof. Mkenda ameelezea azma ya serikali kuendelea ya kuboresha viwango vya elimu na mafunzo, hasa katika maeneo ya ujuzi.
Ameainisha maeneo ya kipaumbele katika ushirikiano kuwa ni pamoja na fursa za kutoa mafunzo kwa vitendo (internship), kubadiili watumishi hususan wahadhiri na wakufunzi ili kuwezesha kutoa mafunzo kwa ufanisi kulingana na kwa soko la sasa pamoja na
kubadilisha teknolojia na ujuzi ” _Technology transfer”_
Mkenda ameainisha sekta za kipaumbele katika mafunzo kuwa ni ujenzi , usafirishaji na Teknolojia. Ambapo ameeleza nia ya dhati ya Tanzania katika kuhakikisha inaandaa wahitimu wenye ujuzi unaokubalika kimataifa.
Kwa upande wake Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa amepokea maeneo hayo na kuwa wako tayari kushirikiana na Tanzania kufanikisha azma ya kuandaa wahitimu wenye ujuzi na umahiri
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania Shegeki Komastsubara na wataalamu wengine kutoka Japan na Wizara ya Elimu na Taasisi zake zinatoa mafunzo ya ujuzi sayansi na Teknolojia.