NA DENIS MLOWE, IRINGA
MAMLAKA ya Mapato Mkoa wa Iringa (TRA) wamekutana ma waandishi wa habari wa mkoa katika semina fupi iliyoambatana na iftari ikiwa na lengo la kujenga mahusiano bora na kuwapatia elimu ya kodi.
Katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa hotel ya Mount Royal iliongozwa na meneja wa Mkoa wa Iringa Peter Jackson ambaye alisema kuwa urahisi wa kulipa kodi unatokana na jamii kupewa elimu na kazi ya vyombo vya habari kulahisisha elimu hiyo kwa watu wengi zaidi kwa muda mfupi.
Alisema kuwa licha ya kutambuana katika kazi wanahabari wakiwa na uelewa wa masuala ya kodi elimu hii itawafikia wananchi kwa uharaka kwa kupitia vvombo vya habari na kusaidia jamii kupata elimu kwa ufanisi umuhimu wa kulipa kodi.
Alisema kupitia vyombo vya habari vikiripoti kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayojengwa na Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupitia kodi inahamasisha wananchi kulipa kodi kutokana na kuona vitu vya maendeleo.
Jackson aliwakumbusha wananchi kudai risiti wanapoununua na wafanyabiashara kutoa risiti wanapouza bidhaa zao kwani bila hivyo watakumbana na adhabu za kisheria za ukwepaji kodi.
Alisema kuwa katika hilo Wanahabari wana uwanda mpana wa kuwaelimisha wananchi namna kodi inavyofanya kazi kupitia miradi na maendeleo katika sekta mbalimbali kama elimu, afya ambazo hujengwa kutokana na kodi.
Naye Afisa Elimu kwa Mlipa Kodi na Mawasilia Mkoa wa Iringa, Shaga Gagunda alisema wajibu wa mlipa kodi lazima ajisajili aidha kuwajibika kuwasilisha marejesho katika kodi ya mapato, au ongezeko la thamani kwa TRA.
Alisema kuwa wadau wanatakiwa kulipa kodi kwa wakati na usahihi ambapo serikali imeweka kulipa kwa awamu, kuwasilisha matamko sahihi na wakati husika jutunza taarifa za kodi kwa miaka mitano .
Alisema kuwa wajibu mwingine ni kudai risiti pale unaponunua au kuuza kutoa taarifa pale ambapo hawatoi risiti kwa tra.
Gagunda alisema kuwa mteja wa TRA upata huduma bila upendeleo kutunziwa siri, anayo haki ya kudhaniwa kuwa mwaminifu na mfanyabiashara anayo haki ya kupinga maamuzi kama hajaridhika nayo katika makadirio
“Kikubwa kufata taratibu za kupinga,ana haki ya kupanga kufanya biashara gani tra hawapangiii mtu Kupata majibu ya malalamiko, kawaida ndani ya siku moja au ndani ya siku tano za kazi” Alisema
Aliongeza kuwa mfanyabiashara asipotimiza wajibu atawajibishwa kwa mujibu wa sheria na huu husababisha wengi kuishi kwa hofu kutokana na kutotimiza wajibu wao na kuanza kukimbiq mamlaka hivyo lipa kodi uishi bila hofu.
Kwa upamde wake mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoa wa iringa Frank Leonard amewashukuru TRA kwa kulitambua kundi la wanahabari na kusema hii itawapa chachu ya kuandika na kuelimisha umma masuala yanahusu kodi.
Alisema kuwa wanahabari wakiandika habari za kodi na wale kwenye radio wakitumia vyombo vyao kutoa nafasi kuhusu elimu kwa mlipa kodi itarahisisha elimu kuenea na kutoa wito kwa TRA kuanza kutoa elimu ya ulipaji kodi ngazi ya shule ya msingi ili wakue wakijua umuhimu wa kodi katika maendeleo ya nchi.

