Kampuni ya Taifa Gas imeendesha semina ya mafunzo ya siku moja kwa wafanyabiashara kwenye soko la feri ya namna bora ya kutumia majiko na mitungi ya gesi kwa ajili ya kupikia.
Akizungumza kwenye semina ya mafunzo hayo iliyofanyika katika soko la feri , Afisa Usalama kutoka Taifa Gas, Henry Muya amesema kwamba matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kupikia , usalama na kulinda afya za watumiaji.
“Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan inafanya jitihada zote ili kuhakikisha kwamba watanzania wanaachana na matumizi ya kuni na mkaa na kutumia nishati safi ya gesi kwa ajili ya kupikia na kulinda mazingira yetu,” amesema Muya.
Ameongeza kwamba ni muhimu kwa wafanyabiashara ikiwemo wa Samaki nchini kujifunza kutumia nishati safi na majiko ya gesi kwa ajili ya kupikia ili kuweza kurahisisha shughuli zao za uzalishaji mali.
“Matumizi ya mkaa na kuni yanaweza kusababisha madhara kwenye mfumo wa upumuaji kwa mtumiaji kwahiyo ni muhimu kwa watanzania kupata elimu ya matumizi ya nishati safi ambayo yanalinda mazingira kwa nchini yetu kwa ujumla,” amesisitiza Muya.
Amesema kwamba nishati safi ya gesi inatoka katika nchini za Uarabuni ambapo kuna uchimbaji wa mafuta ili soko la nishati safi linaendelea kukua kwa kasi sana kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
“Kwa matumizi ya majiko ya gesi yanasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi ya fedha na kuokoa muda wa upikaji wa chakula sehemu za biashara na majumbani,” aliongeza Muya.
Kwa upande wake , Katibu wa Soko la Feri, Nassoro George Mbaga amesema kwamba ni muhimu kwa watanzania kuendelea kutumia nishati safi na salama kwa ajili ya kutunza mazingira.
“Nachukua fursa hii kuwashukuru sana kampuni ya Taifa Gas kwa semina hii kwa wafanyabiashara wa soko la feri na ni matumaini yangu kwamba elimu hii waliyoipata leo wataweza kuwapa na wenzao,” alisema Mbaga.
Amengeza kwamba nishati safi na majiko ya kupikia ya gesi ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa biashara kwa wafanyabiashara wa soko la feri na kukuza uchumi wa nchini husika.

