Meneja wa Tanesco Mkoani Mara Nickson Babu amewatoa hofu wakazi katika Manispaa ya Musoma waliokumbwa na maafaa ya Nyumba kuezuliwa na upepo kuwa shirika hilo linafanya kila jitihada kuhakikisha umeme unarejea katika maeneo ambayo nguzo zimeangushwa na upepo.
Kauli hiyo ameitoa Wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema wamesambaa maeneo yote kuhakikisha huduma inarjeshwa mara moja huku akiwataka wananchi kuacha kuwasha vyombo vya umeme Wakati huu wakifanya jitihada ya kurejesha nishati hiyo.
“Kwanza tuwape pole wateja wetu hali nimbaya kuna nguzo zimeanguka naimetulazimu kuzima umeme ilikuweka hali ya Usalama kwahiyo tutahakikisha masaa 24 tuko kazini wateja wetu kuhakikisha tunawarejeshea huduma”Mhadisi Nickson Babu Meneja wa Tanesco Mkoani wa Mara.
Babu alisema maeneo mengi yameathilika na nguzo kuanguka baada ya upepo na mkali kuvuma na Mvua kunyensha nyakati za Usiku.