Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Usangu Foundation na On Africa Construction Niazhan Ibrahim amekabidhi zawadi mbalimbali yakiwepo majiko ya Gesi kwa washindi wa mashindano ya Quraan
na kuwakumbusha washiriki kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhubiri amani ya nchi
Ibrahim aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipozungumza
katika mashindano ya tatu ya Quraan yaliyoandaliwa na Taasisi ya Umatul Islamiyya ya Gongol a Mboto Jijini Dar es Salaam
Alisema mashindano ya Kuhifadhi Quraan ni kielelezo cha kuwepo kwa Uhuru wa kuabudu nchini na kisema kuwa anawakabidhi zawadi hizo za mitungi ya Gesi,sabuni za kifulia na vifaa mbalimbali Vya Shule kama mchango wa Taasisi katika kuthamini Quraan
“Mashindano ya Kuhifadhi Quraan ni kielelezo cha kuwepo kwa Uhuru wa kuabudu nchini na kwamba Uhuru huo unatokana na upendo baina ya watu wote,” alisema Ibrahim na kusisitiza Jamii hususan waislamu kuendelea kushikamana kwa pamoja bila kujali itiladi za kidini ili kuimarisha umoja na amani ya taifa
Aidha amewasihi wazazi na watoto walioshiriki mashindano hayo sambamba na WA Tanzania wote hususan waislamu kuacha kuchochea vurugu na badala yake Kila mmoja aone umuhimu wa kuhubiri amani
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Taasisi iliyoandaa mashindano hayo na mwalimu wa AL Madrasat
Umatul Islamiyya Abdulaziz Ismaili alisema lengo la kuanzishwa kwa Taasisi hiyo ilikuwa ni kuwajenga watoto katika kuisoma dini na Kuhifadhi Quraan
Alisema tangu Taasisi hiyo ianze rasmi mwaka 2018 mpaka sasa wamefanikiwa kuwa na jengo lenye ghorofa tatu na tayari wamezindua Madrasa ambayo inafanya vizuri katika kazi ya kuwalea watoto kwenye misingi ya imani
“Tangu Taasisi yetu ianze rasmi mwaka 2018 hadi 2020 tumefanikiwa kuwa na jengo letu la ghorofa tatu na tumezindua madrasa ambayo mlezi wake ni Alhaji Ibrahim Ismail,” alisema Ismail
Katibu pia aliyataja mafanikio ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo kuwa ni pamoja na
Kushirikisha madrasa zingine katika kutoa changamoto katika madrasa yetu
Kuongeza idadi ya washiriki kila mwaka.
Kufikisha watoto juzuu saba ambao leo hii wameshiriki wa tano
Mashindano kujulikana na kutangaza kituo chetu kama kitovu cha elimu na vitendo.
“Taasisi imeweza kifanikisha kujenga msikiti wa kuswalia kwa harambee ndogondogo.
Kuanzisha mashindano ya wakina mama juzuu moja na mbili ambao leo wameoatiwa zawadi zao.
Pia kufanya mikusanyiko ya wakina mama ndani ya kila ramadhani na matokeo haya ni kuwa na uhusiano ulio mzuri baina ya viongozi na wakina mama.
Alisema Taasisi yao inatarajia kufanya mashindano ya aina kila mwaka.
kuanzisha mfuko wa kujikwamua kiuchumi ,kuanzisha mashindano kiwilaya ambayo yatapanda hadi kufikia daraja la juu,
kusaidia wasiojiweza mayatima na wajane.kuanzisha program itakayo muwezesha mtoto kujisomea hata akiwa amechelewa madrasa.kufungua kituo cha watoto yatima ndani ya mwaka huu.
Pia kuanzisha Shule ya awali itakayo mjenga kijana kimaadili na kufikia ngazi ya daraja la kwanza
Hata hivyo alizitaja baadhi ya changamoto Taasisi inanokabiliana nazp kuwa ni pamoja na kutopata wadau wa kutosha kuchangia mashindano hali ambayo husababisha kusuasua kwa mashindano