Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Machi 25, 2025 amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Haikainde Hichielema katika Ikulu ya Rais iliyopo Jijini Lusaka Zambia.
Rais Hichielema amemshukuru Rais Samia kwa ujumbe huo maalum na kubainisha ya kuwa Zambia na Tanzania ni nchi zenye historia na ushirikiano wa kindugu muda mrefu na usio na mipaka.
Waziri Mhagama akiwa ameambatana na ujumbe wake akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Generali Mathew Edward Mkingule amemshukuru Rais Hichielema kwa mapokezi mazuri na ushirikiano imara ulipo baina ya Tanzania na Zambia.