Na Pamela Mollel,Arusha
Mhashamu Baba Askofu Mkuu wa kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (K.K.A.M)Oscar Ulotu amemsimika rasmi Dkt.Philemon Mollel,mfanyabishara maarufu(Monaban) kuwa Baba Askofu Mteule wa Dayosisi ya Arusha
Baba Askofu Mollel amesimikwa Machi 23,2025 kwenye ibada maalum iliyofanyika katika kanisa la K.K.A.M Mto wa Mbu-Kigongoni Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha
Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali na vyama vya Siasa,waumini pamoja na kwaya mbalimbali ambazo zilitumbuiza katika hafla hiyo iliyokuwa ya kipekee
Akizungumza wakati wa kumsimika Askofu Mkuu,Oscar Ulotu ambapo alimkabidhi fimbo kama ishara ya kuongoza waumini wa kanisa hilo,alimkumbusha Askofu Mollel kuwa fimbo hiyo siyo ya kuchapa watumishi au waumini bali ni fimbo ya kuwaelekeza na kuwarudisha kwa Mungu
“Fimbo hii siyo ya kuchapa bali au kuwakaba itasaidia katika kuwaelekeza wanapokosea na kuwarudisha taratibu kwa maombi”Anasema Askofu Mkuu Ulotu
Pia aliwataka Watanzania kwa ujumla tunapoelekea katika uchaguzi mkuu mwaka huu kuendelea kuombea Nchi iweze kudumisha Amani,Upendo na Mshikamano
Akizungumza mara baada ya kusimikwa rasmi Baba Askofu Mollel wa Dayosisi ya Arusha,anahaidi kutoa ushirikiano ili kuendeleza kazi nzuri ya kumtumikia Mungu
“Ninahaidi kufanya kazi ya Mungu kwa moyo na watu wategemee kupokea nguvu za Mungu,Amani na furaha Katika kumtumikia Mungu”Anasema Askofu Mollel
“Mungu wetu ni wamipango amepanga mimi kuwatumikia wananchi,nilishaendaga kwenye siasa na nilihitaji kuwatumikia lakini Mungu amenichagua nimtumikie kwa nafasi hii niliyoipata leo”Anaongeza Askofu Dkt Mollel
Naye Askofu Dkt.Edward Mwaikali kutoka Mbeya ambaye alihubiri katika ibada hiyo anawashukuru waumini pamoja na wachungaji wa kanisa hilo kwa kujitokeza kwa wingi,pamoja na kuwepo kwa kiongozi wa Dayosisi hiyo kuondoka siku za hivi karibu,lakini wameweza kushikana pamoja na kutunza umoja wa Kanisa
“Askofu Mollel amesimikwa leo,ninamfahamu vizuri,anaupendo mkubwa lakini pia anahofu ya Mungu anauwezo mkubwa wa kuleta watu pamoja,naamini ataweza kufanya kazi nzuri katika Dayosisi ya Arusha kwa kuwa amegusa watu wengi pamoja na wenye uhitaji katika jamii tumuombee sana kazi hii ni ngumu”Anasema Askofu Dkt Mwaikali
Pamoja na mambo mengine,Askofu Mkuu aliweza kuzindua jengo la Ofisi ya Parokia ya Mto wa Mbu-Kigongoni iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 26 huku wakipanda miti katika eneo hilo ikiwa ni utunzaji wa mazingira.