Happy Lazaro, Arusha
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ,John Mongela ametoa rai kwa jumuiya ya Umoja wa wazazi kupata muda wa kutosha wa kuwaelewesha wananchi kutambua umuhimu wa amani, mshikamano na utulivu uliopo ndani ya Taifa.
Ametoa rai hiyo Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Emmanuel Nchimbi wakati akifungua kongamano la kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Suluhu Kwa kutimimiza miaka minne ya mafanikio katika uongozi wa Taifa.
“Mafanikio ni kitu kimoja lakini Amani na mshikamano huu umechangia Kwa kiwango kikubwa sana kupata maendeleo haya” amesema.
Amesema kuwa katibu Mkuu balonzi nchimbi ameeilekeza Jumuiya ya Wazazi kulibeba swala la kukamasisha amani na mshikamano pamoja na kuwa mfano wa kudumisha amani ,ulinzi na usalama katika maeneo yao hasa katika kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi.
“Tudumishe Amani ulinzi na usalama katika maeneo yetu hata kama tutategeshewa Ili tuweze kugafilika na kuingia kwenye fujo sisi tuwe imara na kuepuka vishawishi hivyo haswa katika kuelekea uchaguzi tuwe mfano wa kuimarisha amani ” amesema.
Aidha amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassani ameasisi falsafa ya R4 ambayo ni lazima watanzania wote tuidumishe Kwa ajili ya kuimarisha zaidi maendeleo na utulivu wa Taifa letu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Taifa Fadhili Maganya amesema kuwa jumuiya ya wazazi inampongeza Rais Dokta Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta maendeleo ndani ya miaka minne tangu aliposhika hatamu za uongozi wake ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya Barabara, miundombinu ya maji, miundombinu ya Afya, ujenzi wa zahanati , na vituo vya Afya pamoja na huduma zingine za kijamii.
Amewaomba wananchi kumuunga mkono , kumtia moyo , kumuombea na kumtakia kila la kheri Dokta Samia Suluhu Hassan Kwa kuwa yupo tayari kushughulikia changamoto za maisha zinazowakabili watanzania na kuzipatia ufumbuzi.
“Mwaka huu tunauchaguzi tuhakikishe kwamba kupitia miundo yetu ya Chama Cha Mapinduzi tuhakikishe tunamuombea tunamtetea na kumsemea Kwa wananchi” amesema mwenyekiti
Naye Katibu Mkuu jumuiya ya Wazazi Ally Hapi ameeleza azimio la Baraza kuu la wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Kwa kumpongeza rais Kwa kutiza miaka minne ndani ya uongozi na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuhakikisha falsafa ya R4 inatekelzwa wa vitendo ikiwemo umoja, mshikamano ikiwemo utekelezaji wa ilani ya CCM pamoja na maboresho kwa wananchi.
“Wajumbe wa Baraza la wazazi tumefanya kikao Cha Baraza kuu la kawaida Jijini Arusha,tumezingatia kazi nzuri alizofanya Rais ikiwemo ujenzi wa miradi ya kimkakati ikiwemo bwawa la Mwalimu Nyerere ambapo mashine tisa you zimewsahwa ikiwemo utuaji wa ndoo kichwani “amesema .
Amesema pia wajumbe wa Baraza kuu walimpongeza Rais Samia Kwa kazi kubwa ya kutekeleza ilani hiyo ndani ya kipindi cha miaka minne ikiwemo kupongeza mkutano mkuu wa CCM Kwa kumchgua Rais Samia kuwa mgombes mteule wa CCM ikiwemo Jumuiya hiyo kuwa mstari wa mbele kuhakikisha ushindi huo unapatikana na jumuiya hiyo ipo tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.