NJOMBE,Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) nchini imeitaka jamii kuacha tabia ya kuficha ushahidi wa matukio ya ukiukwaji na uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na ndugu ama8 jamaa wanaotekeleza vitendo viovu vikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto unaofanywa ndani ya familia na badala yake waripoti vitendo hivyo katika mamlaka husika ili sheria ichukuliwe dhidi ya watekelezaji.
Rai hiyo imetolewa Dkt. Thomas Masanja Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
Wakati akitoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora kwa wananchi, maafisa usafirishaji,abiria wa kituo cha mabasi mjini Makmbako
Wilayani Njombe ambapo amesema kesi nyingi za ubakaji na ulawiti zinakufa kwasababu ya watu wanamalizana kifamilia na kuacha muathirika kwenye matatizo makubwa
Hivyo wakati umefika sasa kila mmoja kutoa taarifa kwa wakati na kushiriki kutoa ushahidi itakapohitajika ili hatua z kiaheria zichukuliwe.
“Kuna watu wanapoteza ushahidi kwasababu matukio mengi yanafanyika ndani ya familia na watu wa jirani, wengine kwa kuogopa kuwafunga ndugu wana amua kuficha ushahidi na mtuhumiwa anaachiwa,hivyo tuache tabia hiyo ili kilinda haki za watoto wetu wanaobakwa na watu wetu wa jirani”,alisema Dkt Masanja.
Kufuatia mafunzo hayo ,washiriki akiwemo Frank Kilumile wanasema yamekuja kwa kuchelewa kwasababu huko mtaani kuna changamoto kubwa sana la ukiukaji na uvunjaji wa haki za binadamu na kisha kushauri elimu hiyo kuanza kutewa kuanzia ngazi za chini za elimu hususani shule za msingi na sekondari.
Awali akizungumzia suala la utawala bora Said Zuberi, Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) amesema wananchi wanapaswa kuhoji na kuwajibisha kiongozi wa serikali hususani mwenyekiti wa kijiji au mtaa ambae hasomi taarifa ya mapato na matumizi kwa wananchi kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria .
Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo Zuberi amesema kila mradi wa umma unapaswa kuanzia chini ili kujua mahitaji ya watu kabla ya kutekeleza badala ya kufanya bila kushirikisha watu hivyo endapo wananchi watakutana na changamoto hiyo pia wanapaswa kuhoji hatua zilizozingatiwa.
Kwa upande wake Magreth Kilawe afisa Mtendaji wa kata ya Kitisi ameishukuru serikali kwa kuwapa elimu wananchi na watumishi wa umma juu ya haki za binadamu na masuala ya utawala bora kwasababu yatasaidia kuongeza uwajibikaji kwa kila mtu.


