Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa mbegu za kilimo ASA Bwn,Leo Mavika wa kwanza kulia akitoa maelezo ya mradi wa Umwagiliaji katika Shamba la Mbegu Ngaramtoni Arusha kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali.
Na Lucas Raphael,Arusha
Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali imeridhishwa na matumizi ya shilingi Bilion 15 .7 ya ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika Hekta 800 za mashamba ya Wakala wa Mbegu za kilimo nchini (ASA) .
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Wakala wa Mbegu Jijini Arusha Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali , Japhet Hasunga alisema Kamati hiyo imeridhishwa na Miradi ya ASA inayotekelezwa katika Shamba la Mbegu Arusha Ngaramtoni linalowekewa miundombinu ya Umwagiliaji Hekta 200,Shamba la Mbegu Msimba kilosa Mkoani Morogoro Hekta 200 pamoja na Shamba la Mbegu Kilimi Nzega Tabora Hekta 400.
Alisema kwamba Kamati imerizika na matumizi ya fedha katika utekelezaji wa Miradi hiyo , kazi ambayo ilifanyika chini ya Tume ya Umwagiliaji.
“Nawapongeza Sana ASA kwa usimamizi wenu mzuri pamoja na Tume ya Umwagiliaji kwa kazi hii” alisema Mwenyekiti wa kamati Hasaunga.
Alibainisha kwamba jukumu la Wakala wa Mbegu za kilimo ASA nikuhakikisha Miradi hiyo inakamilika kwa wakati nakuanza shughuli ya Uzalishaji wa Mbegu unaongezeka kwa kasi kwani serikali inatengemea uzalishaji uongezeka mara dufu na kuzalisha kipindi chote cha mwaka na kusambaza mbegu hizo kwa wakulima wa mazao mbalimbali .
Alisema matarajio ya serikali ni kuona Uzalishaji unaongeezaka ilikumudu soko la ndani na mpaka kuuza Nje ya nchi kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali katika wizara ya kilimo.
Aidha aliipongeza wizara ya kilimo Kwa kuwa na mipango madhubuti ya kuhakikisha inaongeza Uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwekeza katika sekta ya Umwagiliaji.
” Niipongeze wizara ya kilimo imefanya kazi vizuri Sana Kwa kuongeza Uzalishaji wa Mbegu na kuongeza uwekezaji uliofanywa na serikali hongeren Sana kilimo” alisema Mh.Japhet Hansunga.
Mjumbe wa kamati hiyo Jacqueline Ngonyani alisema Miradi hiyo ya Umwagiliaji ya Wakala wa Mbegu za kilimo inapaswa kuleta tija ya kuongeza Uzalishaji wa Mbegu bora kwa wananchi.
Alisema Wakala inapaswa kujitangaza kwa kutoa elimu kwa wananchi ilikuwa na soko kubwa la Mbegu ikiwa ni pamoja na kutafuta soko la Nje ya nchi ili kuongeza kipato cha kujiendesha.
Kaim Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA,Leo Mavika aliipongeza Kamati hiyo Kwa kukagua Miradi ya Umwagiliaji na kuridhishwa na ujenzi unaoendelea.
Alibainisha kuwa Wakala wa Mbegu utaendelea kutekeleza maagizo yote yaliagizwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali katika Miradi Ili lengo la serikali liweze kutimia la kuongeza Uzalishaji wa Mbegu.
Mavika alisema mahitaji ya Mbegu Nchini ni Tani 127,650 ambapo hupatikani wa Mbegu ni mchache hivyo jitihada za kuhakikisha Uzalishaji wa Mbegu zinaendelea kwa kuimarisha Umwagiliaji.
Alisema Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Kwa kushirikiana na Tume ya Umwagiliaji itaendelea kusimamia Miradi hiyo Kwa umakini mkubwa ili iweze kuleta tija kwa jamii na serikali hasa kuongeza Uzalishaji.
Aidha aliiambia kamati hiyo kuwa katika Shamba la Mbegu Ngaramtoni Arusha eneo lililowekewa miundombinu ya Umwagiliaji ni Hekta 160 kati ya 200 huku utekelezaji wa kazi ikiwa ni asilimia 82, Shamba la Mbegu Kilimi eneo lililowekewa miundombinu ya Umwagiliaji ni Hekta 220 kati ya 400 sawa na asilimia 60 huku Shamba la Mbegu Msimba ufungaji wa center pivot (3) tatu kati ya sita unaendelea.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa alisema Miradi hiyo inaendelea vizuri ipo katika hatua za mwisho wa ukamjlishaji licha ya kuwepo kwa changamoto.
Alisema Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itaendelea kumsimamia mkandarasi iliakamilishe kazi Kwa wakati tayari kwa kuanza kufanya kazi ya Uzalishaji wa Mbegu.
“Tume tumepokea maelekezo yote na sisi tutaendelea kumsimamia mkandarasi iliakamilishe kazi Kwa wakati kama mikataba inavyo sema.” alisema Mndolwa ..
Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wizara ya kilimo Dkt.Hussein Omary alisema kama wizara wataendelea kusimamia maelekezo yote ya Kamati kwa Taasisi ilikuhakikisha kazi zinakwenda vizuri.
Alisema ukamilishaji wa Miradi hiyo mkubwa ya Umwagiliaji utaongeza tija kubwa ya Uzalishaji wa Mbegu Nchini nakupunguza uagizaji wa Mbegu kutoka nchi za Nje.
” Malengo ya wizara nikuhakikisha tunaongeza Uzalishaji wa ilikupunguza ama kuacha kuagiza Mbegu kutoka Nje hivyo tuna kila sababu ya kuhakikisha tunasimamia vizuri Miradi hii ikamilike kwa wakati tuanze Uzalishaji ” alisema Dkt Omary.
Kaim mtendaji Mkuu wa wakala wa mbegu za kilimo ASA Bwn,Leo Mavika wa kwanza kulia akitoa maelezo ya mradi wa Umwagiliaji katika Shamba la Mbegu Ngaramtoni Arusha kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali.